Thursday, 28 November 2013

Kuna ukweli wowote katika hili? Wabongo waishio majuu kwa sifa!!?

Jamani tuache utani baadhi ya Wabongo (waTanzania) waishio nje ya nchi wanamisifa usipime. Yaani kama umebahatika kutembelea nchi za UK na USA au nchi zinazofanana na hizo nchi basi utanielewa ninachotaka kuongelea hapa…wakiwa wabongo kwa wabongo wanapenda sana kuzu ngumza kiswahili na sana sana wakikutana na mtu wa nyumbani (Tanzania) ambaye amekwenda au umekwenda kwa shughuli zako maramoja basi ndiyo kabisaaa yaani wakikuona tu wanapenda sana kuzungumza au kuongea kiswahili na wewe.

Ila cha ajabu na kushangaza mtu huyo huyo au watu hao hao warudipo bongo kuja kusalimia ndugu au kwa majukumu fulani fulani basi hawataki au hataki kabisa kuzungumza kiswahili na badala yake anaongea ung'eng'e kuanzia mwanzo hadi mwisho au maneno 10 ung'eng'e na mawili kiswahili.

Sasa mimi najiuliza inakuwaje unapokuwa nchi za ung'eng'e unapenda kuongea lugha ya nyumbani kwenu Tanzania alafu ukirudi Bongo kwa mapumziko ya wiki mbili au mwezi hutaki kuongea kiswahili.

Ukienda shopperz plaza unajifanya yes no,mlimani city yes no,kwenye daladala yes no ukikutana na washikaji zako wa kitambo yes no nk nk nk. Sasa hii yote ni nini? ni ushamba au ndiyo unataka tujue kuwa unatoka USA au Ulaya?

0 maoni: