Monday, 28 October 2013

Pole WEMA SEPETU


Baba mzazi wa Muigizaji maarufu nchini Wema Sepetu aka Beatiful Onyine , Balozi Isaack Abraham Sepetu, amefariki dunia siku ya jana baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari  na kiharusi na kulazwa  katika hospitali ya TMJ kwa muda mrefu. 


Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarag Nyerere.  Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.

Mpaka mauti yanamkuta Balozi Isaack Abraham Sepetu alikuwa ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya uwekezaji wa vitega uchumi, Zanzibar. 

"Bwana litoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana lihidimiwe"

0 maoni: