Wednesday, 23 October 2013

Full aibu Mke wa mtu na Mume wa mtu wafumwa gesti usiku wa manane

ILE Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers imeshuhudia mume wa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Benedict na mke wa mtu aitwaye Rehema ambao wamenaswa laivu wakifanya ‘mambo’ gesti. Wawili hao walinaswa hivi karibuni kwenye gesti ambayo pia ina baa iitwayo Blue Roze maeneo ya Buguruni-Sokoni jijini Dar wakijiachia kwa raha zao.

Habari zilizopenyezwa katika timu yetu ni kwamba, baa hiyo hutumia vibaya leseni yake ya biashara kwa kugeuza gesti hiyo danguro ambapo machangu hufanya biashara ya kuuza miili yao katika eneo hilo.
Ilielezwa kuwa baa hiyo huwahifadhi machangudoa ndani yake huku biashara ya ngono ikifanyika mchana kweupe na usiku kucha bila kushtukiwa.
KAZI YAANZA
Ikiwa imebeba kauli ya Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kuhusiana na kukomesha biashara ya madanguro jijini, vijana wa OFM walitinga ndani ya baa hiyo kama wateja na kukamilisha uchunguzi wao ambao uliwapa jibu moja tu – biashara ya ngono inafanyika nje nje!

Wakati huohuo, kijana mwingine wa OFM aliingia upande wa gesti iliyopo ndani ya baa hiyo ili kupeleleza bei zake huku mhudumu akiahidi kupunguza bei kwa kuwa alikuwa na changudoa kutoka ndani ya baa hiyo tofauti na wengine waliokuwa wanatoka nje ya eneo hilo.
TAARIFA POLISI
Baada ya kujiridhisha kuwepo kwa hali hiyo, OFM ilitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ilala, Lucy Kakulu ambaye haraka alimtaarifu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi ambaye muda mfupi baadaye aliwasili kituoni hapo na kutoa baraka kwa OFM na kushiriki kuwachagua askari shupavu wa kufanya oparesheni hiyo.

Ilipotimia usiku wa manane, ndipo zoezi zima lilianza kwa mmoja wa mapaparazi wetu kuingia ndani ya baa hiyo na kupitiliza moja kwa moja hadi ndani ya gesti.
Akiwa ndani, paparazi huyo alifanikiwa kupatana na mmoja na kuingia naye chumbani huku akitoa ishara kuwa kila kitu kilikuwa wazi ni kiasi cha zoezi kufanyika tu.
KAZI IKAANZA
Kufumba na kufumbua askari shupavu wa Kituo cha Polisi  Buguruni, Dar sambamba na timu ya OFM waliingia mzigoni ambapo waliwanasa machangudoa na meneja wao aliyekuwa akizagaa ndani ya gesti hiyo.

Katika pekuapekua hiyo ndipo mume huyo wa mtu akanaswa laivu chumbani na mke wa mtu huku wote wakiomba msamaha kwa kuwa wana familia zao, hoja ambayo haikuwa na nguvu.
KILA MTU ANA NDOA YAKE
Katika kurusharusha miguu, mwanaume huyo alisema anaomba sana ishu hiyo iishie hapo, isifike polisi wala kwenye vyombo vya habari kwani ana ndoa na familia hivyo itakuwa ni aibu kubwa.

“Chondechonde mimi nina ndoa na familia jamani. Sijui nitaweka wapi sura kwa aibu. Naombeni tuyamalize kiutu uzima,” alisikika mwanaume huyo akijitetea kwa polisi, utetezi ambao haukumsaidia. 
Katika mahojiano huku kondom zilizotumika zikiwa zimezagaa kila kona, kwa upande wa mwanamke alikiri kuwa alifanya tendo hilo bila kinga.

“Hatujazitumia sisi hizi, tumezikuta humuhumu chumbani. Lakini nawaombeni sana, msinipeleke polisi nina ndoa yangu. Naombeni mnisamehe kwa sababu mume wangu atanirarua. Ninyi wenyewe mnajua ndoa ilivyo ngumu, tafadhali naomba mnisitiri,” alisikika mwanamke huyo.
SAFARI YA POLISI
Pamoja na kuomba sana, polisi hao waliokuwa makini na kazi yao wakionekana kumuunga mkono vilivyo Kamanda Kova, waliwatilia ngumu na kuamua kuondoka nao wakiwa na pingu mikononi mwao.

Mbali na hao, oparesheni hiyo pia ilimtia nguvuni meneja wa eneo hilo, Emmanuel Mpinge, ambao wote kwa pamoja walifikishwa kituoni na kufunguliwa kesi yenye namba  BUG/RB/13114/2013 - KUFANYA VITENDO VYA UMALAYA 19/10/2013.
Angalia picha zaidi za tukio hili zaidi
Kwa hisani ya GPL

0 maoni: