Ndio, katika ulimwengu wa sasa ambako tatizo la upungufu wa nguvu za kiume limeendelea kuwa donda ndugu, madada wengi wamekuwa wakijikuta katika sintofahamu ya kuwakubali wavulana/wanaume pindi wanapowatokea, wengi wakiamini kuwa huenda nao ndio wale wale, watawanukisha shombo tu halafu mambo yanaishia hapo. Lakini unadhani kuwa ni wote wenye kuwa namna hiyo? Hapana, sio wote wako hivi kwa hakika, lakini je, unamjua vipi mwanaume ambaye atakuwa bora pindi utapoamua kumvulia nguo yako ya mwisho ya ndani?
Kwa msaada wa machapisho mbalimbali ndani na nje ya mitandao, hapa ni vitu vitano ambavyo mwanamke akivicheki, vinaweza kumpa walau uelekeo wa ni kwa kiwango gani jamaa anaweza kuwa bora kitandani.
1. Ni mwenye utu (Gentlemen)
Katika mahusiano na mapenzi kwa ujumla, ni vitu vidogo vidogo sana ambavyo hujenga uimara wa mahusiano na mapenzi baina ya wawili. Je, anakufungulia mlango mnapotaka kuingia au kutoka kwenye gari? Je, anakusaidia kusogeza kiti mnapotaka kukaa au kuondoka mahali mlipokuwa mmekaa? Anakupigia simu kutaka kujua siku yako ilikuwaje, anakumbuka kuhusu kazi yako kubwa ambayo ulimwambia ilikuwa inakusumbua? Hizi huwa ni ishara za mtu mwenye kukuwaza na wataalamu wa mahusiano wanaeleza kuwa, kama anaweza kuwa mwenye utu nje ya kitanda, basi anaweza kuwa zaidi ya mwenye utu muwapo kitandani.
2: Anajua umuhimu wa miguso:
Wanaume ambao kwa kawaida wanapenda kushika shika wasichana kwa minajili ya kuwalainisha kwa ajili ya tendo lenyewe tu, huwa hawapendeleo kufanya hivyo bila sababu maalum, ambayo ndio hiyo ya kutaka kumlainisha mtu kwa ajili ya kumaliza haja zake. Mwanaume mwerevu ni yule mwenye kujua umuhimu wa kumgusa, kumshika na hata kumpapasa mpenzi wake ndani na nje ya kitanda. Kwahiyo kama unaye mtu ambaye mkiwa kwenye meza ya mkahawa mnasubiri chakula, atakushika mkono, atakukumbatia kiunoni wakati mnapita mahali, au kushikanisha mikono yenu wakati mnakatiza mahala fulani kwenye umati wa watu, fahamu kuwa, mwanaume huyu atakuwa anajua kukugusa kwa namna ya kipekee kitandani.
3: Hajitangulizi yeye:
Kwa baadhi ya wanaume, mnapokutana habari kuu huwa ni kuhusu yeye tu. Nini alifanya, nini anataka kula, wapi anataka kwenda na mambo kama hayo. Unadhani hii ni shara ya nini kama sio ya kujijali zaidi yeye huko ndani? Angalia sana mwanaume ambaye mnapokutana tu, kitu cha kwanza anakueleza ni kukuuliza kuhusu siku yako, anapendelea muende kwenye mkahawa ambao wewe unaupendelea zaidi hata kama yeye haupendi. Huyu ni mtu ambaye kwake yeye wewe ni priority, na kwa hakika atakupa hadhi hii zaidi pindi mtapokuwa kitandani. Atakusikiliza unavyotaka wewe na sio anavyotaka zaidi yeye
4. Hana Haraka:
Wanaume ambao wana matamanio juu ya mwili wako zaidi ya wewe mwenyewe, huwa wanaharaka sana ya kukipata wanachokitaka, na wala hawakujali wewe. Hawa huwa tayari kufanya lolote lile ili waupate mwili huo kwaharaka iwezekanavyo. Tofauti anayokuwa nayo mwanaume ambaye ana nia ya dhati ya kuwa mpenzi wako, ni mwenye kuelewa kuwa binti aliye bora sana kwake, ana thamani ya kumsubirisha kwa muda flani na wala hatojali. Kimsingi, huyu ni mtu ambaye pia hupenda apewe muda wa kusimamisha msingi kwa utaratibu na si haraka, kwani nia yake sio kujenga banda la msimu, bali maskani ya kudumu. Ikiwa mwanaume atakutamkia "twaweza kusubiri" au "Hapana, sina haraka za kihivyo", basi tambua kuwa huyu mtu yuko tayari kufanya uwekezaji wa kutosha katika tendo lenyewe.
5: Anakufanya ujisikie wewe ni mrembo na bora:
Ufanyaji mapenzi ambao huwafanya walioshiriki tendo hilo kumaliza huku kila mmoja akiwa anajihisi kuwa dunia nyingine, ni kitu cha kujivunia sana maana mwisho wa siku, wataalamu wanasema kuwa, hiyo ni ishara ya kuwa mwenza wako anakukubali mno. Ndio, kama hakukubali unadhani angekupa ushirikiano hadi wewe uzame dunia nyingine? Mwanaume ambaye anaweza kukufikisha katika hatua hii, kwa kawaida huanza kuonyesha dalili hizi wakati wa maandalizi. Mtu mwenye papara huwa hana muda wa kutosha wa maandalizi, na ikiwa unajikuta unapagawa kwa maandalizi yake tu, fahamu kwa hakika kuwa, huyu si mtu wa kukuangusha kamwe pindi mtapoingia kwenye mtanange wenyewe.
Ikiwa una maoni kuhusu andiko hili, usisite kuwasiliana na Counselor kupitia info@jukwaahuru.com, na ujumbe wako uwe na somo la MAONI au SWALI, kulingana na unachotaka kupata.
0 maoni:
Post a Comment