Friday, 30 August 2013

Kumbe ndio mchezo wake! Aliyempiga Chupa AUNT EZEKIEL ndiye aliyemchana LULU Viwembe

Yvonne
IMEVUJA! Mtuhumiwa aliyempiga chupa mwigizaji Aunt Ezekiel Jumapili iliyopita nje ya Ukumbi wa Bilicanas ndiye aliyewahi kumchana viwembe mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwaka 2011.


Data za Ijumaa zinaonesha kuwa, mwaka 2011 Lulu alivamiwa na wadada wa mjini baada ya kunaswa katika pozi tata na mwanaume wa watu maeneo ya Kariakoo, jijini Dar. Alipoulizwa juu ya sakata hilo, Lulu alitiririka hivi: “Naweza kumkumbuka mwanamke mmoja, namfahamu kwa jina la Yvonne, alinivamia na kuanza kunishambulia huku mkononi akiwa ameshika wembe...”


Mwishoni mwa wiki iliyopita, Yvonne huyohuyo ndiye aliyedaiwa kumpiga chupa mkononi Aunt ambapo haikubainika mara moja sababu za kufanya tukio hilo. Aunt alipelekwa katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni na kushonwa nyuzi sita huku mtuhumiwa akishikiliwa na polisi.

Aunt Ezekiel

LULU


Kwa hisani ya Imelda Mtema/GPL


Related Posts:

  • Meneja wa Wema Sepetu afunguka kuhusu mahusiano yake na Wema MARA  nyingi amekuwa akionekana karibu sana na msanii wa filamu mwenye jina kubwa Bongo, Wema Isaac Sepetu. Ukaribu wao umewafanya baadhi ya watu kuhisi tofauti. Wapo waliosema ni wapenzi kutokana na picha zao za ki… Read More
  • Mmiliki wa Home Shopping Centre hali tete HALI ni tete kuhusiana na tukio la bilionea Said Mohamed Saad kumwagiwa tindikali, athari ni kubwa. Jinsi alivyoharibika inatia simanzi lakini kumpata mhusika wa unyama huo ni kitendawili kinacholitega Jeshi la Polisi Tanz… Read More
  • Kaseja: sijasaini Lupopo, bado naipenda Simba KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja amesema hajasaini mkataba wa kuichezea FC Lupopo ya DR Congo ila wapo kwenye hatua nzuri ya mazungumzo lakini akasisitiza kuwa bado ana mapenzi na klabu yake ya zamani ya Simba. Ka… Read More
  • Mke afumaniwa live..... tena kwenye chumba chao cha kulala! TIMBWILI zito limeibuka baada ya mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samora kumnasa ‘live’ mkewe Hadija akimsaliti kwa kuvunja amri ya 7 (usizini) na hawara ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tena kwenye chumba chao, Ij… Read More
  • Redio ya SHAROimenifanya mauzauza MSANII wa Kundi la Green Masage, linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya TBC, Daniel Mmasi ‘Face Brown’ amefunguka kuwa redio ya marehemu Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ aliyoinunua, imemletea mauzauza Akizungumza… Read More

0 maoni: