Wednesday, 25 September 2013

Uingereza na Marekani kusaidia Kenya

Wataalamu wa kuchunguza mauaji kutoka nchini Marekani na Uingereza wamejiunga na kikosi cha wataalamu nchini Kenya kudadisi hali katika jengo la Westgate. Katibu wa baraza la mawaziri, Francis Kimemia amesema kuwa wataalamu wa Kimataifa watasaidiana na wale wa Kenya kuchunguza jumba hilo na kusisitiza kuwa Kenya itaongoza shughuli hiyo.

Alisema kuwa jumba la West Gate limekabidhiwa kwa wakuu wa ujasusi kwa shughuli zaidi za udadisi.
Kupitia kwa urusa wake wa Twitter, Kimemia amesema kuwa maafisa wataendesha shughuli ya kuondoa vifusi ili kuodoa mmili iliyonaswa katika jengo hilo.
Jengo la Westgate lilitekwa na magaidi Jumamosi mchana huku wakiwaua watu kiholela na kuwateka baadhi.
Takriban watu 61 waliuawa na magaidi hao wakiwemo maafisa sita wa usalama huku washukiwa wengine 11 wakikamatwa.
Bwana Kimemia amesema kuwa Rais Uhuru Kenyatta ameitisha mkutano maalum wa mawaziri hii leo kuhusu shambulizi hilo.
Kwa hisani ya BBC Swahili

0 maoni: