Monday, 19 August 2013

Malinzi achukua fomu ya urais TFF

ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Yanga SC, Jamal Malinzi amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27, mwaka huu. Fomu hizo zilianza kutolewa juzi. Jumla ya wagombea 25 katika nyadhifa mbalimbali wameshachukua fomu.

Taarifa iliyotumwa jana na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, ilisema ukiachana na Malinzi, mwingine aliyejitokeza katika nafasi ya urais ni Omari Nkwarulo, wakati kwenye umakamu wa rais kuna Wallace Karia na Ramadhani Nassib.

Wambura alisema waliochukua fomu za ujumbe ni Athumani  Kambi, Charles Komba, Davis Mosha, Elias Mwanjala, Eliud Mvella, Epaphra Swai, Farid Nahdi, Hussein Mwamba, Jumbe Magati, Kamwanga Tambwe, Khalid Mohamed, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Omari Walii.

Wengine ni Samwel Nyalla, Shaffih Dauda, Stanley Lugenge, Twahir Njoki, Vedastus Lufano, Venance Mwamoto na Wilfred Kidao.

Kwa upade wa Bodi ya Ligi, aliyechukua fomu ni mmoja tu ambaye ni Hamad Yahya, anayeomba kuwania uenyekiti.

Wakati huohuo, Wambura amesema mechi ya Ngao ya Jamii iliyozikutanisha Yanga na Azam juzi, imeingiza Sh milioni 208 zilizotokana na kuhudhuriwa na mashabiki 26,084.


Kwa hisani ya Hans Mloli/GPL

Related Posts:

  • Ndoa ya THEA and MIKE yavunjika? SIKU chache baada ya ndoa ya mwigizaji, Ndubagwe Mithayo ‘Thea’ kuvunjika, mwigizaji Deogratius Shija ‘Shija’ ameibuka na kueleza maumivu anayoyapata juu ya tukio hilo. Akizungumza na Amani hivi karibuni, Shija alisem… Read More
  • Jeuri ya fedha: Mke anunua TALAKA kwa milioni 4 Maharusi katikati wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa bibi harusi (kushoto) na wazazi wa bwana harusi (kulia). UNAWEZA kusema ni jeuri ya fedha baada ya  mwanamke, Rukia Apach kukubali kulipa shilingi milion… Read More
  • Penzi la AFANDE SELE na MAMA TUNDA kwisha? Picha ya familia: Kutoka kulia ni Asha Shiengo ‘Mama Tunda’, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, Asantesana Selemani na Tunda Selemani. KUCHA za Shetani zimeugusa uchumba wa muda mrefu kati ya msanii Selemani Msindi ‘Af… Read More
  • RAY, CHUCHU HANS laivuuuu AMA kweli penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Hatimaye uliokuwa uhusiano wa chini kwa chini wa nyota wawili wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans, siyo siri tena baada ya wahusika hao wakuu kujiachia ‘l… Read More
  • Apofuliwa macho kwa kutembea na mke wa Polisi AMA kweli haki hakuna. Katika hali ya kusikitisha sana, kijana mmoja Elias John, mkazi wa Kigamboni jijini Dar, (28) amejikuta katika wakati mgumu wa kupofuka baada ya kuchomwa sindano inayodaiwa kuwa na sumu kufuatia ku… Read More

0 maoni: