Monday, 12 August 2013

Kaseja akumbwa na balaa lingine! Rais Lupopo amuita paspoti yake yaibwa

KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja, ameendelea kukumbana na mikasa lukuki baada ya paspoti yake kuibwa katika hali ya utatanishi huku rais wa Klabu ya FC Lupopo, Victor Kasongo Ngoy, akimtaka aende DR Congo wiki hii. Habari za uhakika zinaeleza kuwa, paspoti hiyo ya Kaseja iliibwa wakati akiwa kambi ya timu ya taifa hali iliyomlazimu kwenda kuripoti katika kituo cha polisi.

“Baada ya kutoa taarifa, Kaseja alianza kufanya mpango wa kupata pasi nyingine, kitu ambacho kiliwashangaza wengi ni kwamba chumba chake kilikuwa kimefungwa. Inaonekana kama kuna watu wanaomfuatilia.

“Maana walitaka asicheze mechi dhidi ya Stars, lakini hata yule wakala aliyetumwa na FC Lupopo kumfuata Kaseja, amekuwa akipata misukosuko kibao bila sababu, hali inayoonyesha kuna watu hawataki kuona anafanikiwa,” kilieleza chanzo cha uhakika.

Alipoulizwa Kaseja kuhusiana na kupotea kwa paspoti yake, alisema yupo katika mikakati ya kupata paspoti mpya lakini akataka kuendelea kukaa kimya.

“Ni kweli, lakini ningependa niendelee kukaa kimya na mambo yaendelee yanavyokwenda,” alisema.

Taarifa nyingine zinaeleza, kipa huyo atasafiri kwenda DR Congo kuonana na rais wa timu hiyo kama atafanikiwa kupata haraka pasi hiyo ya kusafiria.

Kipa huyo amekuwa akiingia katika misukosuko mfululizo hali inayoashiria kwamba kuna watu walitaka kuona hachezi katika kikosi cha timu ya taifa na ikiwezekana asipate timu ya kuichezea. Kaseja yupo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba na FC Lupopo.


Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • JOHARI: SITEGEMEMI MABUZI KAMA MASTAA WENGINE   STAA wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa hategemei wanaume kama wanavyofanya mastaa wengi wa kike Bongo.Akipiga stori na paparazi wetu  hivi karibuni jijini Dar, Johari amewataka… Read More
  • NGASSA akata Mzizi wa Fitina...... atua Mazoezini Yanga HATIMAYE kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (pichani), amekata mzizi wa fitna baada ya kuanza kujifua rasmi na timu hiyo, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu asajiliwe. Awali kulikuwa na utata wa mchezaji huy… Read More
  • Full aibu PADRE afumwa laivu na mke wa mtu gesti KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu, Ijumaa Wikienda lina sakata zima.&… Read More
  • WEMA anaswa na Mwanaume TATA   STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu amezua gumzo baada ya kunaswa akiwa katika  mikao ya ajabuajabu na mwanaume ‘tata’ maarufu kwa jina la Anti Bilal Mashauz.Ishu hiyo ilipigwa chabo na paparazi wetu Alhamis… Read More
  • DOTNATA alishwa sumu? OOH my God! Mjasiriamali ambaye ni staa wa filamu na muziki Bongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’ amedai kulishwa sumu kupitia juisi na kumsababisha hali yake kuwa mbaya, Amani lina taarifa kamili. Habari za uhakika zili… Read More

0 maoni: