Friday, 23 August 2013

Gwiji Gurumo ang’atuka

1940: Alizaliwa Kisarawe, Pwani 
1960: Alianza muziki 
Bendi alizopiga: Kili Chacha, Kilwa Jazz, Rufiji Jazz, DDC Mlimani, Safari Sound na Msondo Ngoma.  
Alama na kielelezo cha muziki wa dansi nchini, mkongwe Muhidin Maalim Gurumo (73) wa Bendi ya Msondo Ngoma, ametangaza kustaafu fani hiyo baada ya kutumbuiza jukwaani kwa miaka 53.
Gurumo aliyeimba mfululizo bila kupumzika tangu mwaka 1960, alitangaza azma ya kuachana na muziki jana wakati akiongea na wanahabari kwenye Ukumbi wa Habari, Maelezo, Dar es Salaam.
Mkongwe huyo, alitaja sababu kubwa mbili za kufikia uamuzi huo, kwanza akisema amelazimika kufanya hivyo kutokana na umri, na pili kuwaachia vijana fursa kuendeleza fani pale alipoacha.
Alisema kutokana na umri alionao, imekuwa vigumu kwake kwenda sambamba na kasi, mabadiliko na mahitaji mapya ya muziki huo, hivyo kazi hiyo amewaachia vijana.
“Muziki umekuwa asili yangu kwa muda mrefu, sasa naamua kustaafu ili kutoa fursa kwa vijana kuendelea kupiga muziki huu,” alisema Gurumo na kuongeza: “Nimestaafu muziki, lakini nitaendelea kuwa mshauri.”
“Kwa kipindi chote cha kusimama jukwaani kutumbuiza, mke wangu alikuwa anakosa fursa ya kuwa na mimi kwa sababu ya kurudi usiku wa manane kutoka kazini,” aliongeza Gurumo.
Gurumo aliyezaliwa Kijiji cha Masaki, Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, aliwataka vijana wanaokuja nyuma ya muziki wa dansi baada ya kustaafu kwake, kuiga muziki wao ambao umeendelea kudumu na kupendwa mpaka leo.
“Kustaafu kwangu kunakwenda sambamba na kuundwa kamati ya kuangalia jinsi ya kunisaidia kama sehemu ya kuenzi mchango wangu katika fani ya muziki,” alisema Gurumo.
Gurumo alianza muziki na Bendi ya Kilimanjaro Chacha mwaka 1962, kisha Bendi za Rufiji Jazz na Kilwa Jazz kufikia mwaka 1963. Mwaka 1964, alikuwa mmoja kati ya waanzilishi wa Bendi ya Nuta Jazz, ambayo ndiyo ilikuwa kiini cha kuzaliwa Msondo Ngoma.
Pia alikuwa mmoja kati ya wasanii waanzilishi wa Bendi ya DDC Mlimani Park mwaka 1987, kisha Orchestra Safari Sound ‘OSS’, na mwaka 1990 alirudi tena Msondo mpaka alipotangaza kustaafu.
Gurumo ametunga nyimbo nyingi baadhi yake ni pamoja na Ukiwa, Upekepeke si mwema, Rudi Jose, Mwana acha wizi, Mama nipeleke kwa baba na Chatu mkali.
Kwa hisani ya Tumsifu Sanga na Kalunde Jamal, Mwananchi  

Related Posts:

  • Okwi: Nitacheza Simba hata bure BAADA ya kufanikiwa kutua Simba, kiungo mshambuliaji mpya wa kikosi hicho, Mganda, Emmanuel Okwi amefunguka kuwa yupo tayari kuendelea kuitumikia klabu hiyo bure. Okwi amesema maneno hayo akimaanisha kuwa yupo tayari… Read More
  • Vigogo wa Fifa,Uefa kikaangoni Maafisa wa Fifa akiwemo Rais wa chama hicho,Sepp Blatter(kushoto) na Michel Platini(Kulia) wamehojiwa kuhusu uhalali wa mkataba wa kuandaa michuano ya Kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 kwa Urusi na Qatar. Rais wa Fifa… Read More
  • Villas- Boas kujiunga na St.Petersberg Aliyekua Kocha wa Tottenham na Chelsea, Andre Villas-Boas ameridhia kuingia mkataba wa miaka miwili na klabu ya Zenit St Petersburg, taarifa za klabu hiyo ya Urusi zimeeleza. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 36, aliyet… Read More
  • LIVERPOOL FANS: "You'll never walk alone". How did this become the teams moto and why? WHAT DOES IT MEAN FOR YOUR TEAM? HOW IMPPORTANT IS IT? IN WHICH CASES IS IT USED, PRINTED... ETC YOU GET THE IDEA... "You'll Never Walk Alone" was originally part of the great American songbook. It was written by Ri… Read More
  • Pistons yamtema Hasheem Timu ya Kikapu ya Pistons imemtema Mchezaji wake kutoka nchini Tanzania, Hasheem Thabeet ambaye amejiunga na Pistons mwezi septemba akitokea klabu ya Philadelphia iliyokuwa imemchukua kutoka Oklahoma City Thunder. Al… Read More

0 maoni: