Thursday, 22 August 2013

Familia ya MASOGANGE yamwachia MUNGU

FAMILIA ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ inadaiwa kumwachia Mungu ishu ya binti huyo kukamatwa na madawa ya kulevya Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa familia hiyo aliyeomba jina lake lisitiriwe, wameamua kumwachia Mungu ishu hiyo kwani ndiye anayejua ukweli.


“Unajua baba wa Masogange (mzee Gerald Waya) ni mlokole, sasa amekabidhi ishu nzima mikononi mwa Mungu kwa hiyo hayuko tayari kusemasema maneno ambayo hayatakuwa na faida,” alisema ndugu huyo.

Habari zinazidi kudai kwamba, mzee huyo aliwahi kuchukizwa na kitendo cha binti yake huyo kujiingiza kwenye sanaa, hadi kuonekana akinengua kwenye muziki.
Hilo liliwahi kubainishwa na Masogange mwenyewe miaka ya nyuma alipohojiwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa) kupitia safu ya Ten Questions (Maswali Kumi) ambapo ilikuwa hivi:

TQ: Inasemekana umetokea kwenye familia ambayo imeiva kidini, walokole, wao wanachukuliaje suala la wewe kuingia kwenye mambo ya kuuza sura tena wakati mwingine kwenye mavazi ya kimitego?
Agnes: Mh! Baba yangu hataki kabisa kusikia mambo ya muziki na niliwahi kukosana naye lakini nalazimisha kwa kuwa ni moja ya ajira.

Jitihada za kumpata baba wa Masogange ziligonga mwamba baada ya namba iliyotolewa na ndugu huyo kutokuwa hewani.
Masogange na nduguye, Mellisa Edward walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakiwa na ‘unga’ kilo 150 aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.


Kwa hisani ya Imelda Mtema/GPL

Related Posts:

  • Wema Sepetu matatani tena? DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa h… Read More
  • NGASSA akata Mzizi wa Fitina...... atua Mazoezini Yanga HATIMAYE kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (pichani), amekata mzizi wa fitna baada ya kuanza kujifua rasmi na timu hiyo, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu asajiliwe. Awali kulikuwa na utata wa mchezaji huy… Read More
  • Dida apigwa dongo BAADA ya hivi karibuni Mtangazaji wa Radio Times, Khadija Shaibu ‘Dida’ kufunga ndoa na mwanaume aitwaye Ezden, mashosti zake wamemtaka kutulia sasa na asijaribu kugeuza ndoa kuwa fasheni. Wakizungumza na Ijumaa kwa… Read More
  • Soma habari kamili ya Bibi Harusi aliyeaga dunia dakika 30 kabla ya kufunga ndoa Bi harusi huyo, Levina Mmassy (23) aliyekuwa mkazi wa Chanika, Handeni mkoani Tanga alifariki dunia Jumamosi ya Julai 6, mwaka huu, majira ya mchana, muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na Kasisi Masawe. PADRI ASUBIRI Tuki… Read More
  • Changudoa anayewatesa Polisi Dar...... MREMBO mwenye ulemavu wa ngozi, Emmily Omari, 23, mkazi Buguruni, Dar anayedaiwa kujihusisha na biashara haramu ya uchangudoa, hivi karibuni alipandishwa kizimbani kwa madai ya kufanya kosa hilo. Emmily ambaye amekuwa aki… Read More

0 maoni: