Friday 26 July 2013

Ndoa yangu ipo mashakani

Habari zenu waungwana!

Naombeni ushauri wenu kwa jambo hili, Kuna mama mmoja mwenye  umri unaokadiriwa miaka 40 nafanya nae kazi sehemu moja ila vitengo tofauti, Kwa ujumla kazi yangu na yake zinategemeana sana kwa hiyo mara nyingi huwa tunaonana sana tunapokuwa kazini , mbaya zaidi yeye  alikuwa mjumbe wa kamati kwenye harusi yangu na alijitoa kwa 100%.
Cha ajabu siku za hivi karibuni ameanza kunifanyia vituko, akiniona mara aje anishike kimahaba tena mbele za watu, mara aniite maneno yote ya kimapenzi,na hivi karibuni amekuwa akiniomba tutoke huku akiniambia hajaduu kama mwezi hivi , jamani nimejaribu kutumia mbinu zote za kusema NO kiistaarabu lakini naona zinagonga mwamba, sitaki kutumia agressive wayz kwani kulingana na kazi zetu  na umri wake iko siku nitahitaji msaada wake na yeye iko siku atahitaji msaada wangu, Kwa sasa ameanza sasa kunipigia simu usiku akijijulia hali,nimekuwa nikipokea simu zake freely kwani waifu kituo chake cha kazi ni mkoa.naanza kupata wasiwasi hali hii ikiendelea hivi si ndoa yangu itakuwa inatetereka?plz naomba msaada wa the best way ku resolve hii kitu bila kuleta chuki,uadui wala maelewano mabaya ya kikazi.

Uncle W

0 maoni: