Monday 3 June 2013

Mimba yamtesa PENNY

TUMEINYAKA kwamba mimba anayotamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa amempachika mpenzi wake, Peniel Mungilwa ‘Penny’, inadaiwa kuanza kumtesa mtangazaji huyo wa DTV, Ijumaa Wikienda linashuka nayo. Habari zisizokuwa na chenga kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mrembo huyo, zilieleza kwamba kufuatia hali hiyo, Penny alikimbizwa kwenye Hospitali ya Regency, Dar wikiendi iliyopita kisha  akalazwa, akachomwa sindano na kutundikiwa dripu.Akizungumzia hali hiyo,
Penny aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli alizidiwa usiku na alikimbizwa hospitali ambapo pamoja na mengine lakini kubwa vipimo vilionesha kuwa alikuwa na malaria. Hata hivyo, habari tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa Penny aliruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri.

Kwa hisani ya GPL

0 maoni: