Monday, 24 June 2013

Mimba ya Penny yatoka?


TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa. Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.

“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.



Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.

Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lililimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Risasi Jumamosi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Risasi Jumamosi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Risasi Jumamosi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Risasi Jumamosi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.


Habari na Imelda Mtema / GPL

Related Posts:

  • Mtuhumiwa ajinywea mbele ya Hakimu KIOJA cha mwaka kilitokea Jumatano wiki hii katika Mahakama ya Jiji ya Sokoine Drive jijini Dar es Salaam, baada ya mkazi mmoja wa Buguruni, Hassan Omary kujisaidia haja kubwa kizimbani wakati akisomewa shtaka lake la uzur… Read More
  • Ufuska wa kutisha HAKIKA wazazi wanaosomesha mabinti lazima wataumia wakisoma kisa hiki kilichojaa ufuska wa kutisha, Amani linakupa kwa undani. Mwanafunzi wa kike aliyetajwa kwa jina moja la Agness, hivi karibuni alijifungia chumbani … Read More
  • Mchezo umechezwa kwenye hukumu ya MASOGANGE? VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ na shosti yake, Melissa Edward wapo huru kufuatia kesi iliyokuwa ikisikilizwa nchini Afrika Kusini ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine ya Sh… Read More
  • Mfanyabiashara maarufu KIMARA afumaniwa nyumba ya wageni aki............ SHETANI anazidi kuiatamia dunia, ulimwengu unawayawaya! Jamaa mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Manfree, mkazi wa Kimara Mwisho, Dar ambaye inadaiwa ni mfanyabiashara wa baa iliyopo Mbezi Mwisho (Mbezi Shamba) anadaiwa kun… Read More
  • Full aibu ..... Mlokole afuniwa live MATUKIO na vitendo viovu vinaendelea kushamiri juu ya uso wa nchi! Kijana anayedaiwa kuwa muumini wa kanisa la kilokole (jina tunalo) la jijini Dar,  Faraji Oti amekutwa na mazito akidaiwa kufumaniwa na mke wa mtu ali… Read More

0 maoni: