Tuesday, 9 April 2013

UWAZI labaini siri nzito iliyotawala kwa mwaka mzima,lapekua orodha ya VIGOGO vinara wa biashara ya Dawa za kulevya

SKENDO kwamba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, anafanya biashara ya madawa ya kulevya, ilitikisa kisha ikapoa, ila sasa Uwazi lipo kwenye nafasi nzuri ya kupasua jipu. Januari mwaka jana, Pengo ndiye alikuwa wa kwanza kutamka hadharani kuwa anaambiwa anauza ‘unga’, kipindi hichohicho, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ambaye alisema wanafanya kazi kisayansi.

“Kama jina la Pengo tunalo kwamba anauza madawa ya kulevya au hatuna, siwezi kutamka kwa sasa, hatutaki kupindisha ushahidi au kuvuruga upelelezi wetu,” alisema Nzowa.

Hata hivyo, hivi karibuni, Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa vigogo wa jeshi la polisi nchini, aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, akasema kuwa suala la Pengo lina utata ila siyo zito.
“Labda mimi nipasue jipu kwamba jina la Pengo halionekani katika orodha ya viongozi wa dini wanaochunguzwa kutokana na kashfa ya madawa ya kulevya,” alisema kigogo huyo.

Aliongeza: “Hata kwenye ule mkanda uliokwenda bungeni, ukionesha wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, Pengo haonekani. Tulishangaa sana aliposema anaambiwa anauza madawa ya kulevya.”...

KUSOMA ZAIDI HABARI HII BOFYA HAPA

0 maoni: