Monday 15 April 2013

SHILOLE achanwa live na mzazi mwenzie.. asema aache uongo

MZAZI mwenziye na staa wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Makala Elias amembomoa staa huyo na kumwambia aache kuungopea umma kuwa alibakwa wakati waliishi naye kinyumba. Akipiga stori na Stori 3, Makala aliweka wazi kuwa anasikitika anapomsikia Shilole akisema kwamba alipata ujauzito baada ya kubakwa wakati walioana na kuachana miaka ya nyuma kabla staa huyo hajawa maarufu.
 “Namsihi Shilole aache kusambaza taarifa kwenye vyombo vya habari na kuwafanya Watanzania wamuone mtoto aliyenaye alimpata kwa njia ya kubakwa wakati alikuwa ameolewa na mimi,’’ alisema Makala ambapo Shilole alikataa kuzungumzia juu ya ishu hiyo akidai ameshazungumza mara nyingi.

Kwa hisani ya - GLP



0 maoni: