Monday, 22 April 2013

Rose Ndauka anaswa kimahaba hadharani

Staa anayefanya poa katika sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amenaswa akiwa kimahaba akifanya mambo ya chumbani hadharani na mchumba’ke, Malick Bandawe, Ijumaa Wikienda limewapiga chabo.Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu, lilijiri wikiendi katika Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo Coco Beach, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya ‘bethidei’ ya mdogo wake Rose, Recho Ndauka.Baada ya kukolea kwa ‘maji’, Rose na mwandani wake walianza kugandana kama ruba huku wakifanyiana vitendo vya  kimalavidavi.Wakati burudani zikiendelea ukumbini hapo, wawili hao walijitenga pembeni na kuanza kumwagiana mabusu mfululizo huku kila mmoja akijitahidi kuzionesha hisia za upendo alizonazo kwa mwenzake, jambo lililowashangaza baadhi ya wageni waalikwa.


“Makubwa haya! Sijawahi kumuona Rose akiwa kimalovee hivi yaani leo ndiyo mara ya kwanza ila kwa upande mwingine wanaendana na wanapendeza sema tu hawataki kufunga hiyo ndoa jamani tuione,” alisikika dada mmoja akijadili na mwenzake.  Pamoja na hayo, sherehe hiyo ya mdogo wake ilitawaliwa na vituko kibao baada ya wageni waalikwa kukolea ‘maji’ kwani kulikuwa na pombe kali tu huku wasichana wakiwa wamevalia vimini vilivyoacha wazi sehemu kubwa za maungo nyeti hasa wakati wakiserebuka hivyo kuwatoa udenda wanaume wakware.


Kwa hisani ya GLP

Related Posts:

  • Ndoa yangu haivunjiki leo wala kesho..... Aunt EZEKIEL MWANADADA anayetamba katika filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa ndoa yake haiwezi kuvunjika leo wala kesho kwani amejipanga kikamilifu. Aunt aliyasema hayo kwa madai kuwa watu wengi wamekuwa wak… Read More
  • Mambo ya Chuma ulete yamtokea MREMBO puani.... MREMBO mmoja, Rukia Omari mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar amebambwa akidaiwa kuiba fedha kwa njia za miujiza eneo la  Bunju Mwanjenje kwenye duka la Wapemba. Imeelezwa kuwa katika tukio hilo, Rukia alichukua fed… Read More
  • Full Aibu NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushi… Read More
  • Mfanyabiashara wa Kihindi adaiwa kumnyonga Mwalimu.... Simanzi, majonzi na masikitiko makubwa yalitawala katika msiba wa Mwalimu Elizabeth Mmbaga, 22, aliyekutwa amefariki dunia chumbani kwake Kimara Baruti jijini Dar, Aprili 15 mwaka huu, Uwazi lina mkanda mzima. Haba… Read More
  • Haponi mtu IMEBAINIKA kwamba kuna mtandao wa askari ndani ya majeshi mbalimbali ya ulinzi nchini na hasa Jeshi la Magereza ambao unajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Uchunguzi wa Uwazi umebaini kwamba tayari orodha ya… Read More

0 maoni: