Friday, 26 April 2013

Full Aibu

NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.
Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi mmoja na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa).

BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ
Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana, aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.


Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo.

Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote kwa pamoja. Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.

ALIKWENDA KUKUMBUSHIA ENZI ZAKE
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo.


Alijitetea kuwa mume wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’ aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini.

Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.


BINTI WA KIGOGO
Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini akiwa kwenye kundi la makahaba.


Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.

MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE
Akijitetea wakati wa kutoa maelezo, binti huyo aliyeonekana mrembo na mwenye mvuto wa ajabu, alisema kwamba alikuwa na ‘boifrendi’ wake na kuwa alitoroka kwao usiku huo.


Binti huyo aliomba chondechonde asipigwe picha kwani endapo itaonekana gazetini basi atakuwa amejipalia makaa nyumbani kwa vile hataeleweka kwa sababu anapatiwa fedha za matumizi pamoja na ada ya shule.

Ukiacha mwanamke na binti huyo wa kigogo, wanawake wengine wengi walikamatwa, wengi wao walikutwa wakifanya vitendo vya ngono mchangani wakiwa ‘pea’.


MACHANGU WAFUNGUKA
Kati ya wote waliokamatwa, wanawake kumi na tano walikiri kujishughulisha na biashara ya kuuza miili ambapo walisema wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.

ACD MUTAFUNGWA ANASEMAJE?

Kwa upande wake OCD Mutafungwa alisema wameamua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi kwa kuvamia eneo hilo.


INSPEKTA SWAI ATIA NENO
Naye Inspekta Swai aliyekuwa ‘front’ katika zoezi hilo alisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kila wiki ili kukomesha vitendo viovu katika ufukwe huo.

NI MATOKEO YA GAZETI LA RISASI
Oparesheni hiyo ilikuja siku chache baada ya gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko, toleo namba 1000 la Jumatano ya Aprili 17-19 kuripoti ufuska unaofanyika katika ufukwe huo usiku wa saa 9 na kuendelea.  

Uchunguzi wa gazeti hilo ulieleza kiundani vitendo vya ngono, usagaji, ubakaji, ushoga na ujambazi vilivyokuwa vikifanyika eneo hilo hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni wakaona kuna kila sababu ya kufumua uozo huo kwa kuwa ni wachapakazi.


Picha zaidi angalia hapa chini









Kwa hisani ya - GLP

Related Posts:

  • FA & JAYDEE waahirishwa show zao kutokana na kifo cha Magwea... KUTOKANA na habari za kufariki kwa Albert Mangwair ‘Ngwea’, msanii ambaye ni mmoja kati ya wana Hip Hop maarufu nchini, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ ametangaza kuahirisha shoo yake ya The Finest iliyokuwa ifanyike leo (Ijumaa).… Read More
  • Majonzi SAKATA la kijana Bonny Fabian Kavishe kudaiwa kumuua kwa kumpiga risasi baba yake, mzee Livingstone Kavishe akiamini ni mwizi sasa ni simulizi ya machozi kufuatia kusomwa kwa waraka mzito ulioandikwa na mtuhumiwa huyo amba… Read More
  • Ama kweli mjini shule! Ombaomba feki anaswa live.... WAKAZI wa mjini Iringa hivi karibuni wameshuhudia kituko cha mwaka baada ya kumnasa mzee mmoja akijifanya ombaomba kwa kuigiza ulemavu asiokuwa nao. Ombaomba huyo feki alijifanya hana mkono wa kushoto na mguu wa kulia… Read More
  • Makubwa yaibuka baada ya siku 13 ya kifo cha Magwea..... BALAA zito! Siku 13 baada ya kifo cha  mwanamuziki wa kizazi kipya, Albert Kenneth Mangwea ‘Ngwair’, ripoti ya daktari inayoeleza sababu halisi ya kifo chake bado utata mtupu kwani haijawekwa wazi, hivyo kuwafanya wen… Read More
  • Kifo cha KASHI... yametimia KIFO cha msanii wa siku nyingi  katika tasnia ya filamu za Kibongo, Jaji Hamisi ‘Kashi’ kilichotokea Jumatatu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kimehitimisha maono ya mchungaji aliyetabiri kuwa mastaa wawili mmoj… Read More

0 maoni: