Wednesday, 13 February 2013

Diamond afunguka kuhusu mafanikio yake kuhusihswa na ushirikina.....

Baada ya maneno mbofumbofu kusambaa kitaa na mtu mmoja ambaye anajihusisha na tiba za Asili (Mganga wa kienyeji) kusema yeye ndio chachu ya mafanikio ya Mwanamuziki Diamondi ...mwenye kaibuka na kukanusha. Diamond kadai kuwa mafanikio yake yametokana na kuwa karibu na mama yake mzazi ambaye  amekuwa mstari wa mbele kumpa support na  baraka kila anapoenda kwenye show zake. Diamond ambaye hata magazeti ya nchi za Africa mashariki likiwemo gazeti la Daily Nation limemtaja kuwa miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava matajiri zaidi, yupo karibu mno na mama yake mzazi na pengine ndio maana anafanikiwa.
Angalia picha hizi chini zikimuonesha Diamond na kundi zima la wasafi  wakipewa baraka na Mama kabla ya kwenda kwenye show


0 maoni: