Bila shaka umewahi kukutana na sura kama hiyo maishani mwako. Hata kama siyo inayofanana hivyo kwa kila kitu, bali ni sura ambayo unaweza kusema inakaribiana nayo, inalandana nayo. Wanaume wenye sura kama hiyo hapo juu, wanajua kuhangaika sana kwenye maisha, ingawa inaonekana kama vile hawana malengo. Wanakuwa na ufahamu mkubwa katika mambo wanayofanya, lakini ufahamu huo hautumiki au kama ni kutumika huwa ni kwa faida ya watu wengine.
Wenye sura hiyo hupenda sana kutanua na hasa katika wanawake na unywaji, labda tu kama wamepata bahati kuingia kwenye imani za kidini na kuzifuata. Lakini kukuta mwenye sura kama hiyo ameingia kwenye dini na kuifuata, ni jambo gumu sana.
Wenye sura hiyo ni watu ‘poa’ sana na wanaelewana na watu wengi kwa sababu ni wazungumzaji na wachekeshaji wazuri. Ni watu wanaojua kupata kirahisi huruma za wengine. Lakini kama wameanza kushtuka na kugundua kwamba, maisha yao hayana maana sana, huwa wakali na wakorofi.
Hata hivyo, kwa watu wenye sura hiyo kushtuka kuhusu udhaifu wa nafsi walionao kwenya maisha yao ni kitu kigumu sana. Kinachowaponza pia ni kule kulewa kwao sifa haraka. Kama ni wasanii, wanakwama pale wanapoanza kuinuka kwa sababu, huwa wanafikiri wamefanikiwa sana kwa kupata sifa kidogo tu.
Kwa mafanikio kidogo sana, huwa wanafikiria kwamba, wamekuwa watu wakubwa sana na wanafahamika sana. Huwa wanataka kuheshimiwa kwa njia yenye kukera. Kwenye uhusiano, hawaeleweki sana. Wanakuwa moto sasa hivi na baridi baadaye – hawajatulia sana.
Lakini wakipatikana na ‘kushikwa’ huwa waume wazuri sana. Lakini kwa upande wa pili, wenye sura hiyo wanatokea kuwa na ghubu baya sana. Ni watu wasiojiamini, tofauti na wanavyoonekana au kuonesha, hivyo kuwabebesha mizigo wapenzi wao ni jambo la kawaida sana. Kwa hiyo, ‘wakishikwa’ hutulia sana na huamua kutojali kuhusu kinachoendelea.
Lakini wanapotokea kuwa walevi, siyo rahisi kabisa kwao kukaa hata na mke, labda wapenzi wa kuokota hapa na pale. Kwa kuwa ulevi wao unatokana na kukata tamaa, huwafanya kuwa wasumbufu sana kwa mtu yeyote anayekuwa karibu nao. Wanapoamua kutumia vipaji na uwezo wao wa kiakili, wenye sura hiyo hutokea kufika mbali sana kimafanikio. Hata hivyo njia yao kwenda kwenye mafanikio ina miiba mingi kwa sababu, wenyewe pia wana mambo mengi………..
Mdau - Mtambuzi
0 maoni:
Post a Comment