Thursday, 17 January 2013

Wadada waliopiga picha za uchi na kujifanya Wanafunzi waangukia mikononi mwa POLISI

Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni linamshikilia mmoja wa wakina dada waliopiga picha za uchi kwa tuhuma za kumdhalilisha mwandishi wa habari wa blog  pamoja DTVbwana Livingstone Mkoi kwa kumtolea lugha za matusi kwa njia ya mitandao ya simu.

Habari za uhakika zilizothibitishwa na mwandishi huyo zilisema kuwa”Ni kweli jeshi la polisi limemkamata mmoja wa wasichana walipoiga picha za uchi ambazo zililipotiwa na blog hii hivi karibuni kwa tuhuma za kunitukana na kunitishia Maisha” 
Aidha akizungumzia zaidi tukio hilo mwandishi huyo alisema kuwa baada ya kupatikana picha hizo za aibu ambazo hazifai hata kuziona alimpigia simu mmoja wa wasichana hao aliyefahamika kwa jina la Editha  Adolf a.k.a Eliza kwa lengo la kubalansi stori na baada ya kumshushia tuhuma hizo aliambulia matusi makali pamoja na vitisho vya kutekwa harafu afanyiwe kitu mbaya ndipo alipojisalimisha polisi na kupewa taarifa OB/903/2013 KUTOA LUGHA YA MATUSI KUPITIA MTANDAO.

Katika tukio hilo  Editha    Adolf a.k.a Eliza ndiye aliyekuwa wa kwanza kukamtwa ambapo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Summit iliyopo Kinondoni Mkwajuni ambapo mtuhumiwa namba mbili aliyefahamika kwa jina la Lukia Laus bado anatafutwa na jeshi hilo ambapo atakapokamatwa ataunganishwa kwenye kesi hiyo.
Aidha akizungumza na mwandishi wetu Mkuu wa Kituo cha Polisi Kinondoni OCD.Mtafungwa alisema kisheria ni kosa kumtishia mtu Maisha pamoja na kutukana .Hayo yote ni makosa, hivyo ni lazima sheria ichukuwe mkondo wake.
 
wasichana hao wamekuwa na tabia ya kujifanya wanafunzi ili wajipatie wanaume wa kishua ambao mara nyingi hupenda wanafunzi.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na Xdjayz umebaini wasichana hao hawasomi popote isipokuwa wanajishughulisha na biashara ya kuuza miili yao.

Imeripotiwa  na Xdjayz
Kwa hisani ya http://freebongo.blogspot.com

0 maoni: