Jamani wenye tabia hizi waache ....... na hii tabia haina cha uzee wala kijana, hebu some hii hadithi uome baba wa watu alivyoumbuka na kuonekana kama taahira.... Denti kakaa kwenye dala dala anaandika sms kwenye simu yake, huku kashika kibegi chake cha shule, Mzee mmoja pembeni akawa anakomaa kuangalia dogo anaandika nini, macho yanamuwasha kwa UMBEA.
Dogo akaamua kubadili sms, akaandika
"Yule nyoka uliyenipa inaelekea hujamtoa meno ya sumu, hapa nilipo anasumbua kwenye begi anataka kutoka, yaani sijui nitafanyaje na alivyo mkubwa. Akitoka ataniletea tabu hadi mimi, hebu tushauriane nafanyaje"
Babu kuona vile akaanza kusogea pembeni na kujikausha km hajasoma chochote. Denti akachukua kibegi akamrushia.
Mzee akaruka dirishani fasta huku akigutia Nyoooookaaaaaaaaa, Naakuufaaaaaaaa!!!!!
0 maoni:
Post a Comment