Jamani hapa ndani mpo! Habari za majumbani kwenu, na watoto hawajambo? na wifi naye hajambo? samahani sikumbuki kama nilibisha hodi na wala sina hakika kama nilikaribishwa ila cha muhimu ni ule ujumbe ninaowaletea...... nina jazba la hili somo la leo kwa kweli linakera sana.... na kama mnaweza kubadilika naomba mbadilike!!! tena mwenye mabadiliko anakuwa bora kuliko yule aliyezaliwa na utashi huo.
Nafikiri maisha ya siku hizi ya watu kugawana majukumu ya kifedha ndani ya nyumba au kusaidiana ni mazuri sana na yanachangia maendeleo kwa kiasi kikubwa..... lakini kuna baadhi ya wanaume wanafanya utaratibu huu uonekane mbaya na kuonekana haifai eti utakuta mwanaume akiona mkewe anasaidia baadhi ya majukumu yeye ndio anaona kapata nafasi ya kuchakachua na kufanya ubazazi wake! utakuta bila aibu ndio kwanza anatafuta kimwana na kujifanya yeye ana hela sana na kumpangishia nyumba na kujifanya kama mzazi wake hapa mjini... inahusu hapa mjini ulimpetea wewe ? wakati huo kila akiguswa ada utasikia sina! mara sijamaliza mkopo Bank inahusu? unapotaka wanawake mia unategemea nini na hela yako ya ngama... unapenda starehe hela huna? Unataka umchakaze yule wa nyumbani kwa kubeba majukumu ya kuhudumia kila kitu wewe huku aaaah unaitwa pedeshee jamani badilikeni!
Wanawake tulipewa adhabu ya kuzaa kwa uchungu hivyo tupeni nafasi ya kuwalea hao tunaowazaa kikamilifu, ikitokea nimepata kazi tunakubaliana kwamba nikafanye kazi tujikwamue na hali ya uchumi, kwanza mila na desturi zetu zinafundisha kuwa ni jukumu la mume kutunza familia kwa asilimia zote hasa financial support, ila kutokana na utandawizi basi sote tunapiga mzigo, ila kina baba mnaposaidiwa sio ndio mnakimbia majukumu yenu asilimia 100!
Imagine, baba hatoi hata hela ya mboga eti kisa mama anafanya kazi, mama huyu huyu anunue nguo za watoto, atoe hela ya matumizi nyumbani, siku nyingine baba anataka mama aweke hadi mafuta kwenye gari kisa eti ayeye alisahau kuchukua hela kwenye ATM jana yake! Uongo mtupu, hela zake ananywea na kuhonga! kila siku kila akiguswa sina hela ! badilikeni
Yaani inatia hasira kweli mkiamka asubuhi wa kwanza kuingia kwenye gari kisa anaogopa kuombwa hela na dada wa kazi! mama ndio anazungukwaaaaa kutoa hela mara ya daftari mara mchango shuleni, mara mafuta ya kupikia! baba yeye nduki kwenye gari anapiga honi ufanye haraka, hapo kasahau kuwa mama alikuwa macho tangu alfarji, na kama akiwa na katoto kadogo kamemsumbua usiku kucha wakati huo wewe umejichomeka kwenye shuka kama husikii na wala hujali unaendelea kumkimbizakimbiza! hamna huruma?
Mkirudi jioni baba hana habari yeye na yupo busy kwenye laptop au simu au TV si kashamaliza kazi anapumzika, mama amemaliza majukumu ya ofisini anaendelea na ya umama kama kawaida hadi saa tano au sita ndio akione kitanda kilipo apumzike, hapo alishaitwa mara kibao akashushe neti baba anataka kulala! Watoto nao wameshamsumbua kiasi cha kutosha, na akigusa kitanda tu baba kamnasa kama super glue jamani muwe na huruma wenzenu sio machine!
Jamani wenye tabia hizo mjirekebishe, unamfanya mwenzio kama gari au mashine? mtu gani unamuachia mkeo majukumu yote hayo unategemea nini? Kama kazini wote mnafanya wewe kila siku hunahela!, unamfanya mwenzako azeeke kwa majukumu na akichoka ndio wa kwanza kutafuta viportable mtaani humuoni aibu? eti utasikia mama nanii nae kashazeeka halafu siku hizi hayupo smart yupo shabi shabi sana na maneno mengi yasiyo na kichwa wala miguu wakati huo unasahau wewe ndio unaomzeesha kwa tabia zako na ubahili usio na mpango hebu badilikeni, kila mmoja atekeleze adhabu yake, baba kula kwa jasho lako, lea familia yako, lipa ada za watoto, lipia umeme, maji na kodi za nyumba, fungua biashara,na mambo mengine ya kibaba sio full kutega na kuuza sura badilikeni
0 maoni:
Post a Comment