LICHA ya siku za nyuma kudai kuwa hajajifungua, msanii wa filamu Bongo, Riyama Ally juzikati alimuanika mtoto wake aliyejulikana kwa jina la Fatma huku akigoma kumuanika mzazi mwenzake.Mpango mzima ulinaswa na paparazi wetu ndani ya Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza Afrikasana jijini Dar ambapo alifika kwa shughuli zake za kisanii.
Akimzungumzia mtoto wake huyo na sababu za kuficha ujauzito wake hadi amejifungua, Riyama alisema hakuona sababu ya kuanika mambo hayo kwani alijua muda ukifika jamii itajua kila kitu.
“Kuficha kwangu sikuwa na nia mbaya ila unajua siyo lazima kumuambia kila mtu unapokuwa na ujauzito lakini Mungu akishakujalia na ukajifungua salama, hapo waweza kuwa muwazi,” alisema Riyama.
Riyama aliongeza kuwa, anafurahi sana kuitwa mama na anaamini mwanaye huyo atakua katika maadili mema huku akiwa mgumu kuanika mwanaume aliyezaa naye.
Kwa hisani ya GPL
0 maoni:
Post a Comment