Monday, 21 January 2013

Dotnata atua na ujumbe mzito toka Nigeria kwa TB Joshua


MSANII mkubwa Bongo, Illuminatha Posh ‘Dotnata’ hivi karibuni ametua nchini na ujumbe mzito kwa maaskofu kutoka kwa Nabii Temitope Balogun ‘TB Joshua’ wa Nigeria alipokwenda kwenye ziara maalumu ya kufunga na kufungua mwaka 2013. Akizungumza na gazeti namba moja la burudani nchini, Ijumaa Wikienda, Dotnata alisema kuwa ana ujumbe ambao angependa kuutoa kwa maaskofu na wachungaji wa Tanzania, ikiwa kama somo kwao ili wabadilike mara moja kama kweli wanatenda kazi ya Mungu.
Dotnata alifunguka kuwa si kama hawajui au anawafundisha kazi lakini anawafikishia somo hilo.


Alisema kwa TB Joshua, maskini, walemavu, wagonjwa na wajane huwa wanapewa mitaji kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

Pia alisema kuwa TB Joshua amekuwa akitoka na wafuasi wake na kwenda kwenye hospitali mbalimbali na kuwaombea wagonjwa na kutoa misaada kwa wasiojiweza tofauti na hapa Bongo ambapo baadhi ya watumishi husubiria kupelekewa wagonjwa na sadaka tu.

Staa huyo wa maigizo na filamu alimalizia kwa kuwasihi watumishi wa Mungu wote waache malumbano na badala yake waungane wawe kitu kimoja ili wadumishe amani nchini.

Kwa hisani ya GLP

0 maoni: