Thursday 20 December 2012

Tabia za wanawake zisizowapendeza wanaume wawapo kitandani…!



Kwa kawaida wanaume hupenda kuwa viongozi pale wanapofanya tendo la kujamiaana na wapenzi wao au wenzi wao, kwa maana ya kuwaelekeza wapenzi wao wawafanyie hivi au vile ili kuongeza ashki ya tendo. Kitu ambacho si rahisi kwao ni kuzungumzia mambo ambayo hayakuwafurahisha wakati wa kufanya tendo hilo, hususan yale ambayo yalimfanya kupoteza msisimko au ashki ya kuendelea na tendo. 


Hapa chini nitaeleza baadhi ya mambo ambayo hayawafurahishi wanaume wakati wanapojamiiana na wenzi wao lakini wanashindwa kusema kutokana na kuogopa kuwakwaza wapenzi wao.

 

1.Kujibu ujumbe wa simu 
Hapa lazima wanawake wakubali kwamba mfumo dume umeshika hatamu. Kama mwanaume atajibu ujumbe wa simu katikati ya tendo au wakati akimuandaa mwenzi wake kabla ya tendo au dakika chache baada ya kumaliza tendo, mwanamke anaweza kuchukulia kitendo hicho kama vile hathaminiwi na mwanaume huyo na atachukulia kitendo hicho kama vile mwanaume huyo anamtumia tu kumaliza matamanio yake ya ngono ingawa hatasema. Lakini kama kitendo hicho kikifanywa na mwanamke, kwa mwanaume atakichukulia kama vile amedharauliwa kupita kiasi na kinaweza kimsababishie kukosa msisismko wa kuendelea na tendo au hata kama akiendelea hatokuwa na ufanisi kama alivyokusudia…….


2.Kutaja jina la mwingine
Kuna wakati mwanamke anaweza kumwambia mpenzi wake wawapo kitandani, kwamba mpenzi wa rafiki yake huwa anamfanyia huyo rafiki yake hivi au vile wanapokuwa kitandani na angependa na yeye afanyiwe hivyo na huyo mpenzi wake. Au anaweza kumwambia mpenzi wake vile alivyokuwa akifanyiwa na mpenzi wake wa zamani waliyeachana na akataka afanyiwe hivyo. Mwanamke……, ni kosa kubwa sana kutaja wanaume wengine ukiwa na mwenzi wako au mpenzi wako kitandani na wala usije akavuta taswira ya mwanaume mwingine unayempenda wakati wa kufanya tendo ili ufike kileleni, kwani unaweza kujikuta ukitaja jina la huyo mwanaume na kuzua balaa. Mazungumzo yako na mashoga zako kuhusu ngono yaweke pembeni kwanza wakati unapojamiiana na mwenzi wako. 


3.Macho kodo kodo
Wanaume wengi hawapendi kukodolewa macho na wanawake wakati wanapojamiiana. Kuna uangaliaji fulani ambao humvutia mwanaume wakati wa tendo, lakini kumkodolea macho mpenzi wako wakati wa kujamiiana humfanya ajisikie vibaya. Kuwa binti wa kawaida. kupepesa macho huku na kule au kufumba macho na kufumbua huku ukirembua ni vionjo ambavyo humvutia mwanaume na kumfanya aongeze ufanisi katika tendo na hivyo kukufikisha kileleni au kufikishana kileleni.


4.Kukwepesha macho
Wapo baadhi ya wanawake hawapendi kabisa kukutanisha macho na wapenzi wao wakati wa tendo, na hujitahidi sana kuficha nyuso zao ili wasikutanishe macho na wapenzi wao. Hilo ni kosa kubwa, wanaume hupenda kuona macho ya wenzi wao hata kwa kuibiaibia kwani hiyo huwafanya wajue kama uko naye kimwili na kihisia au unawaza mambo mengine. Kumbuka kwamba macho huongea na kwa kukutazama tu japo kwa kijicho pembe mwanaume anaweza kujua kwa usahihi kabisa kwamba unawaza nini……… 


5.Kumwacha mwanaume gizani
Wanawake wengi huwaacha wanaume gizani pale ambapo hawakuridhishwa na tendo. Badala ya kumweleza mwenzi wake kwa upole na kwa lugha nzuri kuwa angependa waendelee na tendo, yeye anakaa kimya huku akionyesha ishara na kunung’unika bila kusema kama hajaridhika na kumwacha mpenzi wake gizani asijue ni kitu gani kimemkera mpenzi wake…….. Sio wanaume wote wenye maono ya kujua lugha ya mwili, hivyo ni vyema kuwa muwazi……. 


6.Kumwambia mpenzi kwamba ulijifunza mahali fulani
Sio vibaya kama utajifunza mambo fulani fulani kuhusu mbinu za kujamiiana kwa ufanisi kupitia magazeti au majarida, lakini si vyema kumwambia mpenzi wako kwamba mbinu fulani na fulani kuhusu kujamiiana ulijifunza kupitia gazeti au jarida fulani. Kufanya hivyo kutamfanya mpenzi wako akuone kama vile wewe sio mbunifu na mtundu kitandani mpaka ukatafute kwenye magazeti. Unaweza kusema, kwani kuna tatizo gani kumwambia mwanaume kwamba nilijifunza mbinu fulani kupitia gazeti fulani aua jarida fulani……… Yeah, inawezekana uko sahihi, lakini hebu fikiria uko na mpenzi wako chumbani mkijiandaa kufanya tendo halafu unamwambia,‘nilijifunza mbinu kadhaa kupitia jarida fulani jinsi mwanaume anavyoweza kumfikisha mwanamke kileleni.’


7.Kuomba radhi kabla ya tendo kwamba ulisahau kunyoa
Kumuomba radhi mwanaume kwamba ulisahau kunyoa nywele za sehemu zako za siri wakati mkijiandaa kufanya tendo kunaweza kumkwaza mwanaume kwa sababu wapo wanaume ambao hupenda sana kujamiaana na wanawake ambao nywele za sehemu zao za siri hazijanyolewa kipara kabisa, kwa maana ndio kwanza zinachipua au zimekua kidogo lakini sio msitu. (Najua si rahisi mwanamke kuacha nywele zake za sehemu ya siri kuwa msitu). Sasa unapomuomba radhi kwamba ulisahau kuvyoa, je unajuaje kama hapendi hizo nywele za chini? Kumbuka kwamba sio kila kinachokukera kuhusu mwili wako kitamkera na mwenzako…………


8.Kusubiri mpaka akuvue nguo
Inabidi wakati mwingine wanawake wajue kwamba wanapaswa kuvua nguo wenyewe bila kusubiri wavuliwe na wenzi wao. Hivi inawezekana kweli unajua kabisa kwamba mnataka kufanya tendo na mwenzi wako halafu unajilaza kitandani na nguo zako ukitarajia aanze yeye kukuvua…! Inashangaza kwamba mwanamke kavaaSkin tight, suruali ya Jinzi na ki- top halafu anasubiri mwanaume aanze kukukuruka na vishikizo ili kumvua nguo mwenzi wake kabla ya tendo. Sio vibaya mwanaume kumvua nguo mpenzi wake lakini ni vyema mwanamke akaanza kuvua mwenyewe na mwanaume akawa anasaidia tu…..


9.Ukimya kupita kiasi: Wanawake wengi wanajisikia aibu kupiga makelele wakati wa tendo. Usifanye hivyo. Wanaume hupenda sana wanawake wanapopiga makelele wakati wa tendo. Naomba nieleweka, sio makelele ya kuigiza, nazungumzia yale makelele yanayokuja yenyewe bila kulazimisha. kwani pale inapokuja hali ya kutaka kupiga kelele kutokana na kunogewa na tendo kisha ukajitahidi kuzuia, ukweli ni kwamba hutalifurahia tendo na badala utaelekeza akili yako katika kuzuia kufanya kile ambacho hisia zinakulazimisha kukifanya………


By Mtambuzi - JF

0 maoni: