Tuesday 18 December 2012

Jack Wolper na Dallas Waanza Kuombana Msamaha

BAADA ya kuachana kwa matukio kadhaa ya kuvurugana msanii Jackline Wolper na aliyekuwa mpenzi wake Dallas, inadaiwa kuwa wameanza kupigiana simu za kuombana misamaha, huku kila mmoja akitoa lawama zake kwa baadhi ya marafiki ambao walichangia kuvuruga mahusiano yao.
Chanzo kimoja cha kuaminika kilichozungumza na mwandishi wa DarTalkkilidai kuwa wawili hao wameanza kupigiana simu za kuombana misamaha na  muda mwingi wawili hao wamekuwa wakikumbushana na kuelezana namna walivyopendana na kufanya mambo yao kwa pamoja ingawa kuna baadhi ya watu ambao waliwapa nafasi ndiyo chanzo cha kuvurunga mapenzi yao. Hata hivyo chanzo chetu bila kusita kilidai kuwa siku tatu zilizopita wawili hao walionana.

0 maoni: