Saturday, 8 December 2012

FAMILIA YAMTEUA KITALE KUSIMAMIA MALI ZA SHARO

 
FAMILIA ya Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ aliyefariki dunia Novemba 26, mwaka huu kwa ajali ya gari iliyotokea Songa-Kibaoni, Muheza, Tanga imemteua msanii wa vichekesho Musa Kitale kuwa mwangalizi wa mali za marehemu, Amani limejuzwa.Akizungumza na paparazi wetu jijini Dar hivi karibuni, Kitale alisema familia hiyo imemteua yeye kwa kigezo cha ukaribu wake na marehemu tangu zamani.

Alisema amepewa jukumu la kuhakikisha mikataba yote ambayo marehemu aliifanya na makampuni mbalimbali inakwenda vizuri sanjari na kuangalia mali kama vile gari na samani za ndani ya nyumba.
“Nimeambiwa nisimamie mikataba, niangalie mali za mshikaji (Sharo) kwa kipindi chote cha kusubiria arobaini ya marehemu ambayo itafanyika Januari 4, 2013 kijijini alikozikwa,” alisema Kitale.
Kitale alisema baadhi ya mikataba anaifahamu kwa vile yeye ndiye aliyekuwa shahidi, “lakini wa DTV  aliosaini siku tano kabla ya kufariki dunia (hakuutaja) inabidi aushughulikie Muddy Suma jamaa aliyemuazima gari marehemu,” alisema.
Kuhusu kwenda kuzima taa katika nyumba aliyokuwa akiishi marehemu, Sinza Palestina Dar, Kitale alisema:
“Kwa kipindi hiki ambacho tunasubiri arobaini ya marehemu ifike ni ngumu mtu kwenda kufungua mlango ili azime taa, namuomba mama mwenye nyumba avumilie kwani zoezi la kufungua mlango wa kwa Sharo ni hadi familia yake iwepo hapa Dar na si mimi peke yangu.”
Akakumbuka jambo hili: “Tulishtushwa na taarifa  tulizozisoma kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi iliyopita kuwa, kuna rafiki mmoja wa marehemu alikwenda pale nyumbani na kutaka kutapeli vitu vya marehemu, kama isingekuwa msimamo wa  mwenye nyumba jamaa angefanikisha utapeli wake ndiyo maana haraka sana familia ikanipa mimi jukumu hili.”


Related Posts:

  • She is back! Kim Kardashianback on track... … Read More
  • Wabotswana wameshamchoka FEZA KESI? When is Feza going Home to Capitalise on BBA fame? I am not asking this question because I am an ‘Oneza’ hater, as some may infer. I am asking because deep down as a (business) woman, I wish for her to prosper. Feza emerge… Read More
  • Umeona kiatu hicho? Read More
  • DIVA aachana na PREZZO? Haya ni maneno ya DIVA kupitia ukuras wake wa jamii...... "Hey Guys Pliz Kwa Heshima Zote na taadhima naomba msiwe mna comment about Huddah Or Prezzo in My Page. That Chapter is closed muda mrefu sana and matter of fact… Read More
  • Mchezo umechezwa kwenye hukumu ya MASOGANGE? VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ na shosti yake, Melissa Edward wapo huru kufuatia kesi iliyokuwa ikisikilizwa nchini Afrika Kusini ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine ya Sh… Read More

0 maoni: