Friday, 14 December 2012

Baby Madaha aumbuka! Adaiwa kodi ya nyumba ya miaka 3 ! apewa notice ya siku 2 ............

 
Wambeya wa mji tumezinyaka  taarifa za kusikitisha kuhusu msanii wa muziki wa kikazi kipya - tunda la Bongo Star Search Baby Madaha ....... Inasemekana Baby Madaha kapewa notice ya siku 2 na mwenye nyumba wake  na hii yote imetokana na msanii huyo kulimbikiza deni kwa muda wa miaka 3 kinachokadiriwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 2 za kitanzania hadi sasa!!!


Nasikia Baby madaha kila siku alikuwa anampa  sound mwenye nyumba wake mara oooh nitakupa  kesho  mara wiki ijayo hali iliyomfanya mwenye nyumba huyo  kuchoka na kumpa notice ya siku 2 ili awe amelipa deni hilo.... kama haitoshi msanii huyo hajaonekana nyumbani hapo maeneo ya Kinondoni kwa siku tatu, na taarifa za notice katumiwa kwa njia ya kilongalonga - simu. 

Inasemekana Baba mwenye nyumba aligadhibika kinoma kiasi  cha kutaka kutoa vitu vya msanii huyo nje lakini kutokana na uvumilivu wake aliacha na aliamua kumpigia simu kuwa anampa siku mbili awe amelipa kiasi hicho cha pesa bila hivyo aondoe vitu vyake.
 


Wambeya hawakukubali wakavuta uzi na kumpata Baby  Madaha na alikuwa na haya ya kusema - Ni kweli taarifa za notice nimezipokea kwa njia ya simu ila hiyo habari ya  kutolala ndani ni ishu ya uongo! Baby aliongeza na kusema sijashindwa kulipa hela hizo lakini nilikuwa na mipango yangu naifanya kwani siwezi kudhalilishwa kwa pesa ndogo kiasi hicho hata kama anaishi kwenye nyumba ya kupanga.

Related Posts:

  • Mtaa wa ngono wafumuliwa.... NI hakika ‘mtaa wa ngono’ umefumuliwa! Sakata hilo lilijiri saa tisa usiku, Ijumaa iliyopita, Barabara ya Shekilango, kuanzia Bamaga hadi Sinza Mori jijini Dar eneo ambalo makahaba wameligeuza chumbani, Operesheni Fichua M… Read More
  • Baada ya Diamond kufichua siri...........Uwoya amwaga machozi KUFUATIA habari iliyoripotiwa na gazeti tumbo moja na hili, Amani wiki iliyopita, ikiwa na kichwa cha ‘DIAMOND AFICHUA KISA CHA KULALA NA UWOYA!’, mwigizaji Irene Uwoya amemfungukia mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnu… Read More
  • Shilole kaiba simu za Diamond? TAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.Msanii huyo alikumbwa na kas… Read More
  • WEMA azua timbwili Wema Isaac Sepetu akiwa amefura kwa hasira. STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi, Amani linakuletea kis… Read More
  • Mtawa Bandia atiwa mbaroni Iringa Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.  JESHI la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru mwenye umri wa miaka 44 aliyevalia mavazi ya kitawa wa masister w… Read More

0 maoni: