Sunday 25 August 2013

Trafiki FEKI atoa viroja mbele ya Hakimu

JAMES Hussein, mkazi wa Kimara, Dar alikuwa na wakati mgumu wa kukwepa kamera zilizotua Mahakama ya Wilaya Ilala, jijini Dar juzi baada ya kufikishwa kwa kosa la kujifanya trafiki.

Tukio hilo lilijiri mahakamani hapo Agosti 22, mwaka huu ambapo mshitakiwa alikana mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi, Joyce Minde.



Trafiki feki huyo alitumia muda mwingi kujificha sura ili kamera zisimchukue lakini alichemsha kwani kila alipojifunua kidogo alikuta kamera ziko mbele yake.


Hali hiyo ilimfanya mshitakiwa huyo aamue kujiachia kwa kutoa kofia aina ya kapelo kichwani na picha za kumwaga kupatikana.



Akisoma mashitaka hayo, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga alisema mnamo Agosti 14, 2013, huko Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, Dar, mtuhumiwa alikutwa amevaa nguo za askari wa usalama barabarani akijifanya ni mwajiriwa wa jeshi la polisi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.


Hata hivyo, mshitakiwa alipelekwa rumande Segerea, hadi Septemba 5, 2013 baada ya kukosa wadhamini wawili kwa shilingi milioni kumi na nne.



0 maoni: