Sunday 25 August 2013

NISHA afunguka kuhusu mahusiano yake na NEY wa MITEGO HAKUNIPATA KIRAHISI

Mwigizaji  wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka na kusema kuwa kiukweli Ney alimpenda sana........na kwa sasa  anajivunia kupendwa na kijana huyo kwani alihangaika sana kumpata. Akizungumza na mmoja wa mapaparazi, Nisha alisema Ney alimfuatilia kwa kipindi kirefu na alimzungusha kama miaka miwili kabla hata hajawa staa. “Nikivuta ile picha ya kumdengulia kiasi kile mpaka kuamua kumkubali, naamini alinipenda tu na hata kama hakunipenda lakini najivunia kwamba alihangaika kunipata,” alisema Nisha. Mapenzi ya wawili hao inasemekana hayakudumu kwa muda mrefu iliwachukua miezi kadhaa   kabla ya kuachana na kila mmoja akichukua time yake.

0 maoni: