Thursday 13 December 2012

Wanawake wenye sura hii hawajali na wanajua kupenda…!

Unaiona sura hiyo hapo juu? Hiyo ni sura ya mwanamke ambaye anacheka. Lakini hata kama angekuwa hacheki, bila shaka ungeweza kuibaini sura yake kama unavyoibaini hivi sasa. Mwanamke mwenye sura kama hiyo ni mwanamke smati sana, yaani anayajua sana maisha. Hii ina maana kwamba huyachukulia maisha kama yanavyokuja. Hukubaliana na kile ambacho kwa wakati huo ndicho kilichopo.

Mwanamke wa sura hiyo ni mchapa kazi na asiyejali sana kuhusu kazi gani anafanya, bora mkono unaenda kinywani. Ni sura ya kipaji na mara nyingi ni kipaji cha usanii au urembo. Anapobaini kipaji chake hufika mbali sana, lakini kwa namna alivyo anaweza kuonewa sana pia.


Ni mwanamke mwenye kujua upendo hasa, yaani akimpenda mtu, hampendi kwa kile alicho nacho na wala hampendi kwa masharti. Kumpenda mtu kwa masharti ni kuonesha upendo kwa msimu tu, yaani pale ambapo mtu amekutendea wema na wewe ndio unatenda. 

Mwanamke wa aina hii hupenda bila kujali ametendewa nini na mpenzi. Lakini akiona mpenzi mwenyewe habebeki huamua kuondoka. Mwanamke wa namna hii huwa hajali sana kuishi mwenyewe, hajali sana kupoteza mpenzi, kama ni lazima ampoteze. Lakini ujue hapo amejitahidi kumsaidia huyo mpenzi hadi kufikia kumpoteza.

Hebu tazama zaidi midomo kuliko sehemu nyingine. Kwa kawaida hiyo ni midomo ya ucheshi na uelewa na ni midomo ya mzaha na masihara mengi yasiyoumiza. Maringo yapo kidogo lakini yanafichwa na huruma. Sura ya namna hiyo ni sura ya huruma na kujibainisha.

Kama mwanaume ametulia na kupata mwanamke wa aina hii anaweza kufurahia sana ndoa yake kwa sababu hatasumbuliwa na vijilawama vya hapa na pale, hatazongwa huku na kule na hataziriwa. Sura hiyo haijui kuzira, inajua kukasirika hapohapo na kugeuza hasira kuwa mzaha. 

Lakini kwa bahati mbaya, kama sura hii imezaliwa na kulelewa kwenye familia yenye majivuno au yenye ugomvi miongoni mwa wazazi, hugeuka na kuwa mtu mwenye majivuno, dharau, hasira za haraka na kutojua kupenda. Lakini hii sio mara nyingi sana. 

Sura hii ni ya mwanamke asiyejali sana kuhusu ngono, hasa kama amelelewa mahali ambapo ngono haikutiliwa nguvu sana. Lakini kama amelelewa mahali ambapo fedha ziliwekwa mbele na ngono ikatajwa kama kitu cha kawaida, hupenda ngono ajabu ya Mungu. Lakini pia idadi ya hawa siyo kubwa sana.

0 maoni: