Monday, 10 December 2012

Halima Mdee- Hali mbaya jimbo la Kawe! Amuweka rumande mwanachama pasipo kosa, Ahusishwa na rushwa!


Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya jimbo la Kawe zinasema kwamba kwa sasa hali ya Mbunge huyo ndani ya jimbo lake na hata ndani ya chama chake ni mbaya kutokana na tabia, uongozi na mwenendo wake mbovu jimboni na hata ndani ya chama, hali iliyopelekea kupingwa vikali na makamanda na wanachama mbalimbali ndani ya jimbo hilo tofauti na ilivyokuwa hapo awali. Habari zaidi zinasema kwamba mbali na tabia ya dharau na majivuno kwa sasa mbunge huyo anafanya kila jinsi kuhakikisha kwamba viongozi wa jimbo waliotimuliwa kwa ubadhilifu na umamluki wanarudi katika nafasi zao za awali ili kuweza kujihakikishia kwamba wanamlinda na kumpitisha 2015 katika wagombea watakaowania ubunge kupitia tiketi ya chadema katika jimbo hilo. Kikiripoti zaidi chanzo hicho kimeeleza kwamba kwa sasa Mbunge Halima Mdee ameenda mbali zaidi na kusema kwamba atamuweka mtu yeyote yule atakayeonekana kuwa kinyume naye kimawazo na kivitendo kama ambavyo hivi majuzi ameweza kumuweka rumande (POLICE OYSTERBAY) Mwanachama hai wa Chadema katika jimbo hilo ajulikanaye kwa jina la Richard Madinda huku akisisitiza kwamba bado kuna Makamanda wengine saba wanaompa wakati mgumu katika jimbo hilo ambao amesema hawamuwezi na anawatafuta ili kupitia wadhifa wake kama mbunge na hela alizonazo awanyooshe. 

Katika upande mwingine Mbunge huyo anahusishwa na kile kinachosemekana kwamba ni kula rushwa na kwa pamoja na mtendaji na viongozi wengine wa eneo la jogoo kuhalalisha uuzwaji wa kiwanja hicho kwa Mbunge mwenzake Mh. Nyambari Nyangwine ambaye kwa haraka tayari ameshazungushia uzio karibu eneo lote la kiwanja hicho ambacho awali kilikuwa kikitumika kwa michezo haswa ule wa mpira wa miguu, mikutano ya kidini, siasa nk. 

Tangu mwaka jana Mbunge Halima Mdee wa Jimbo la Kawe amekuwa katika mchuano mkali na Makamanda wa chama hicho ndani ya jimbo lake na hata kufikia kujihusisha na mbinu chafu za kununua na kupandikiza Viongozi wake wa jimbo ambao Wanachama na viongozi wa jimbo, kata, matawi na mashina katika jimbo hilo ilihali Wananchi hawawataki hiyo ikiwa ni katika kile kinachoonekana kuwa ni hatua za awali za Mbunge huyo kuitetea nafasi yake ya Ubunge mnamo mwaka 2015.

0 maoni: