Sunday 9 December 2012

Vitu ambavyo huwapagawisha wanaume wamwonapo mwanawake.......!



1Sura nzuri yenye mvuto 
Lakini isiwe imesiribwa mavipodozi mpaka inachusha, inatakiwa iwe na simple make up za kiushakaji na macho yawe mazuri na yawe yanavutia hasa pale unaporembua. 



2. Tabasamu 
Leo ngoja niwape siri, hakuna kitu kinachowavutia wanaume kama tabasamu la mwanamke. kama mwanamke anataka kumshawishi mpenzi, basi tabasamu iwe ndio nyenzo muhimu. mwanaume huwa hapindui kwa mwanamke mwenye tabasamu bashasha.



3. Unywele 
Nywele huwa zinawaangusha wanawake wengi, unakuta mwanamke kashupalia mtindo huo mmoja wa nywele kwa mwezi mmoja.. Hee hauna hela ya saloon? inatakiwa kama umedumu na mtindo mmoja wa nywele basi isizidi wiki moja, lakini mwezi...! hiyo si sawa kabisa. kwa taarifa yenu nywele huwa zinawavutia sana wanaume hasa zinapokuwa zimetengenezwa kwa umahiri mkubwa. jamani eh msije mkatengeneza nywele mkapitiliza, ipo mitinndo mizuri ya nywele ambayo inafaa hata kuingia nayo maofisini. usitengeneze nywele mpaka unakuwa centre of attraction. hiyo siyo kabisa.



4. Kivazi 
wanawake wengi huchemsha katika mavazi, yapasa kila mwanamke ajue ni mavazi gani yanaendana na mwili wake, sio ukimuona mwenzio kapendeza na kivazi flani na wewe unakurupuka. siku hizi ukienda kwenye maduka ya nguo maaarufu kama Boutique unakutana na wataalamu wanaoweza kukushauri mavazi gani yanakupendeza kulingana na mwili wako. watumieni ili msije tia aibu mkipata ki date.



5. Kiatu 
Kiatu nacho kina mvuto wake, wanaume wengi hupenda kuchunghuza aina ya kiatu alichovaa mwanamke kabla ya kutoka naye. kuna wanawake wengine wanapenda kuvaa viatu ambavyo vinawapa shida kutembea, unakutana na mwanamke kavaa kiatu kirefuuu eti anaenda na wakati lakini akitembea kama ngongoti...mweh..! tafuta kiatu ambacho kitakufanya uwe huru kutembea utakavyo......



6. Makalio
Naamini hata wanawake wenyewe wanajua ni kiasi gani wanaume wanafagilia sana makalio au kishuzi kama vijana wa mjini wanavyoita. wanaume hawapendi makalio makuubwa sana, wanapenda makalio ya wastani, na kama mwanamke amejaaliwa kalio kubwa, basi inabidi awe makini na aina ya mavazi atakayokuwa anavaa... asipendelee mavazi yatakayokuwa yanamshepu sanaaa. anatakiwa kuwa na mavazi yatakayoweza kumsitiri makalio yake yasimchore kivilee.................

0 maoni: