Tuesday 11 December 2012

Chezea Cocaine wewe!!!!!!!! RAY C apata nafuu.. Familia yake yatoa shukrani kwa JK

RAY akimshukuru Rais

Rais kwenye picha ya pamoja yeye , familia yake na Rais

Mwanamuziki machachari enzi fulani RAY C aka kiuno bila mfupa inasemekana karecover kale kaugonjwa kake ka uteja.Baada ya kutumia madawa na kuharibika kabisa  Mama yake mzazi aliomba msaada kwa Watanzania baada ya kuhisi yeye na familia yake wameshindwa! Mungu si Athumani kilio kikafika Ikulu na  Rais JK Kwa huruma akajitolea kulipia  gharama za matibabu na sasa hali ya mdada huyo imeanza kurudi kuwa sawa... kutokana na  mafanikio ya afya  Familia akiwemo RAY C mwenyewe , Mama yake mzazi na Dada yake jana walitia timu Ikulu na kusema asante kwa JK.
Angalizo
Jamani Masuper star wa kibongo hii iwe fundisho kwenu, leo JK kaguswa kesho ataguswa nani? na isitoshe haya ni mambo ya kujitakia wanaacha kusaidiwa wenye matatizo muhimu zari limemwangukia yeye mwenye matatizo ya kujitakia badilikeni kwani ukiwa maarufu lazima ujiingize kwenye mambo ya ajabuajabu?

0 maoni: