Friday, 15 August 2014

Mkono wa rubani wang'oka hewani


Rubani mmoja nchini Uingereza alipoteza mwelekeo angani akiendesha ndege ya biria baada ya mkono wake wa bandia kuchomoka wakati alipokua akielekea kutua.
Rubani huyo wa shirika la ndege la Flybe mwenye umri wa miaka 46 , aliruka kutoka uwanja wa ndege wa Birmingham, akiwa na abiria wapatao 47 ndani yake, wakati alipokaribia kutua katika uwanja wa ndege wa mji wa Belfast alikumbana na upepo mkali angani ambao ulimsababisha atue kwa ghafla ilivyo bahati hakukuwa na madhara kwa ndege yenyewe wala abiria.

Katika maelezo aliyoyatoa baada ya manusura, mkurugenzi wa shirika hilo la ndege la Flybe Captain Ian Baston, anayehusika pia na masuala ya usalama katika shirika hilo la Flybe alimuelezea rubani kiongozi wa ndege hiyo aliyekua akiiongoza kuwa ni mwenye uzoefu wa hali ya juu na mwenye kuaminiwa pindi awapo angani, na hivyo usalama wa abiria na wahudumu huwa katika mikono iliyo salama sana .

Muda mfupi tu kabla ya kuielekeza ndege Dash 8 kutua kwa dharula rubani huyo alijikagua na kuona kwamba mkono wake bandia wa shoto ulikua sawa lakini baada ya tukio hilo ghafla akajikuta mkono huo umechomoka.

Ndege hiyo ilitua kwa mlio mkubwa ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa na pia ndege haikuharibika.

Rubani alisema atakuwa makini zaidi katika siku za usoni kuhusiana na mkono wake huo bandia.

Kwa hisani ya BBC Swahili

Related Posts:

  • Mwizi wa kutumia bodaboda auawa KIJANA mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayedaiwa ni mzoefu wa wizi kwa kutumia usafiri wa pikipiki ‘bodaboda’, ameuawa baada ya kumliza mwanamke aliyetambulika kwa jina la Jusmini. Tukio hilo … Read More
  • Ipe maneno picha hii Read More
  • LEMA abaka? BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo (pichani) anamtuhumu mbunge mmoja ‘mtata’ wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne Makinda (jina tunalo) kuwa amembaka, Uwazi lina kisa cha aibu ya … Read More
  • Barua ya mapenzi toka kwa Brother man .... Chezea Kiinglish wewe? Dalling , Me Love u. if u loveng and i will hepi. also when look u i filling my hurt moves fast fast like woch clock. wen to drinking wota in glas cup me i seen you pikcha u looked very goodsome. plizi answer me likwest t… Read More
  • Mashetani yavamia shule ya Sekondari Manzese Wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam jana wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu kutanda … Read More

0 maoni: