Wednesday, 26 March 2014

Vigogo wa Fifa,Uefa kikaangoni

Maafisa wa Fifa akiwemo Rais wa chama hicho,Sepp Blatter(kushoto) na Michel Platini(Kulia) wamehojiwa kuhusu uhalali wa mkataba wa kuandaa michuano ya Kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 kwa Urusi na Qatar. Rais wa Fifa, Blatter na Platini wa shirikisho la soka barani ulaya Uefa, walishiriki katika mchakato huo mwezi Desemba mwaka 2010.Mkuu wa kitengo cha upelelezi ndani ya Fifa anafanya uchunguzi namna ambavyo mchakato huo ulifanyika.
umla ya Wajumbe 13 kati ya 24 waliokuwa kwenye kamati wamekuwa wakihojiwa kuhusu sakata hilo.
Baadhi ya walioshiriki kupiga kura wamestaafu huku wengine wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa halikadhalika kushinikizwa kuacha kazi baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria ya Fifa.
Hatua hii haina uhusiano na uchunguzi uliofanywa na gazeti la Daily Telegraph kuhusu maafisa wa zamani wa Fifa, Mohamed Bin Hammam na Jack Warner wanaohusishwa na utoaji wa mkataba wa kuhodhi mashindano ya Kombe la dunia kwa Urusi mwaka 2018 na Qatar mwaka 2022.
Juma hili, gazeti hilo limeeleza kuwa shirika la upelelezi FBI linachunguza malipo yanayodaiwa kutolewa na Kampuni ya Bin Hammam kwa Warner na Watoto wake muda mfupi baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika.
Kwa hisani ya BBC Swahili

Related Posts:

  • Kaseja akumbwa na balaa lingine! Rais Lupopo amuita paspoti yake yaibwa KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja, ameendelea kukumbana na mikasa lukuki baada ya paspoti yake kuibwa katika hali ya utatanishi huku rais wa Klabu ya FC Lupopo, Victor Kasongo Ngoy, akimtaka aende DR Congo wiki hii.&nb… Read More
  • Biggest Beauty No-No's Christina hit the great trifecta of beauty fails with this one: over bronzed, invisible brows and sparse spider lashes. …to over powdering. Blend, blend, blend! Keep your lipstick from bleeding with an outer liner i… Read More
  • Yanga wamuongezea adhabu Mrisho Ngassa? IMEFAHAMIKA kuwa Klabu ya Yanga, ndiyo iliyochangia ukubwa wa adhabu aliyopewa kiungo wake mshambuliaji Mrisho Ngassa, Championi Ijumaa limebaini. Taarifa hiyo inakuja wakati ambao Ngassa amefungiwa kucheza mechi sit… Read More
  • Madawa ya Kulevya yamfilisi AISHA MADINDA WIMBI la uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya limeshika kasi hivi sasa kwa wasanii na watu mbalimbali huku Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe akilivalia njuga kulikomesha.Wakati hayo yakiendelea, mnenguaji aliyetik… Read More
  • Malinzi achukua fomu ya urais TFF ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Yanga SC, Jamal Malinzi amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27, mwaka huu. Fomu hi… Read More

0 maoni: