Monday, 27 January 2014

Mchumba wa mtu anaaga anakwenda kwa bibi yake kumbe anaenda kuuza mwili!

OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers si mchezo! Safari hii imenasa tukio la mchumba wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Jose kuuza mwili. Tukio hilo lilijiri eneo maarufu la Baa ya Kaumba iliyopo katikati ya mji kwenye Mtaa wa Makongoro, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo OFM na polisi walikuwa kwenye oparesheni za kufichua uovu wa biashara haramu ya ngono.Kwa mujibu wa mchumba huyo katika mahojiano na OFM, aliaga kwao Kilosa kuwa anakwenda Morogoro mjini kumuuguza bibi yake ambaye ni mgonjwa.

Tofauti na matarajio ya familia yake, mrembo huyo alikwenda kukita kambi maeneo hayo akijihusisha na biashara hiyo haramu eti kwa madai ya kusaka fedha ya kununulia sare za harusi yake ambayo inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.
Jumatano iliyopita, OFM ilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye alieleza kuwa kuna ‘shori’ ambaye ni mchumba wa mtu anajiuza katika viunga vya Kaumba.
Dada huyo aliendelea kueleza kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe katika kikao cha harusi ya dada huyo huku akiwa ameshachangia shilingi elfu 50 lakini alishangaa kumuona maeneo hayo hatarishi.
“Niamini mimi, tunakaa naye Mji Mpya (Morogoro). Hata fedha za advance ya ukumbi, vinywaji, MC na muziki tumeshalipa na harusi yake inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.

Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.

OFM ikishirikiana na polisi wanaojua kujituma kwenye majukumu yao walimtia mbaroni dada huyo akiwa katika pilikapilika zake za kunasa wanaume huku mmoja wa vijana wa OFM akijifanya mteja na kupatana naye bei ya kuingia chumbani kwa ‘shoti taimu’.
Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.

“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.

Hata hivyo, kilio chake kiligeuka cha samaki kwani hakikusikika, yeye na wenzake walionaswa walipelekwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha polisi ili kupisha sheria ichukue mkondo wake.   
Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • RAY C anajuta kumjua LORD EYES........... Rehema Chalamila ‘Ray C’ akiwa na Lord Eyez enzi hizo. INAWEZEKANA umekuwa ukisikia vitu vingi kuhusu lejendari wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ lakini hukupata chansi ya kumsikia mwenyewe akifunguka mwanzo mwis… Read More
  • Huu ndio Utajiri wa Marehemu Askofu KULOLA NI maswali tata yameibuka baada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evengelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Dk. Moses Samuel Kulola (85) kwamba, ameacha utajiri wa kiasi gani wakati wa uhai wake, Uwazi… Read More
  • Ndoa ya Mzee MAJUTO chali! MWANAMKE anayedaiwa kufunga ndoa ya siri na mchekeshaji mahiri Bongo, Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto au King Majuto, Rahma Abdallah (20 - pichani), ameibuka na kudai kutelekezwa na mumewe huyo. Ndoa hiyo ambayo… Read More
  • Daz Baba Kwishey MASKINI Daz Baba! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia habari ya kusikitisha ya msanii huyo ambaye jina lake kamili ni David Jacob kunaswa akiwa amezima mjini hapa huku ulevi wa kupindukia ukidaiwa kuwa chanzo. Daz Baba … Read More
  • DIAMOND ampa mimba mtoto wa shule na kuingia mitini...... MREMBO aliyetimuliwa shule akiwa kidato cha nne baada ya kutundikwa mimba, Sasha Juma ameibuka na madai kuwa amezaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. MCHEZO MZIMA - Habari kutoka kwa chanzo ch… Read More

0 maoni: