Saturday, 14 December 2013

Penzi la AFANDE SELE na MAMA TUNDA kwisha?

Picha ya familia: Kutoka kulia ni Asha Shiengo ‘Mama Tunda’, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, Asantesana Selemani na Tunda Selemani.

KUCHA za Shetani zimeugusa uchumba wa muda mrefu kati ya msanii Selemani Msindi ‘Afande Sele’ na Asha Shiengo ‘Mama Tunda’  ambapo inadaiwa sasa kila mmoja yuko na ‘hamsini’ zake, Ijumaa linaibumburua. Kwa mujibu wa chanzo chetu, kutoelewana kwao kunachangiwa na kucheleweshwa kwa ndoa baina yao pamoja na mambo mengine ambayo hakuwa tayari kuyaanika. “Kwa kifupi mapenzi sasa hivi kati ya Afande na Mama Tunda ni ‘vululuvululu’, kila mmoja yuko kivyake.
“Chanzo kikubwa ni kucheleweshwa kwa ndoa ambapo Afande anaonekana kupotezea suala la kuoana ,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa  jina lake gazetini.

Mwandishi wetu alipomtafuta Afande Sele kuweka wazi juu ya tuhuma hizo, kwa sauti ya upole kabisa alikiri kutokuwepo maelewano baina yake na mzazi mwenziye huyo huku akishindwa kubainisha haswa chanzo cha kutengana kwao.
“Ni kweli, kwa sasa siko na Mama Tunda, mimi niko Morogoro na yeye yuko Dar,” alisema msanii huyo bila ufafanuzi wa ziada.

Hata hivyo Mama Tunda alipotafutwa kwa njia ya simu, alissema chanzo cha mambo yote ni kutovalishwa pete ya ndoa.

“Chanzo ni hicho tu, nimechoka kukaa kwenye uchumba kwa muda mrefu ni miaka 15 sasa, hadi Tunda amefikisha miaka 13, si ni ajabu hiyo na sasa tuna mtoto wa pili ambaye ana miaka 2 bado ni wachumba tu, nimechoka,” alisema Mama Tunda na kisha kukata simu.
Wawili hao wamejaliwa watoto wawili, Tunda Selemani (13) na Asantesana Selemani (2).

Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • Hodi hodi wana hot n town! Mie ni mdada  wa makamo naishi Dar es salaam .... shida yangu kubwa naombeni msaada wa kujua maeneo gani ya mwili wa mwanaume yakiguswa au kufanyiwa chochote yanampa raha muhusika  k… Read More
  • Ten Reasons Why Sex Should Wait Until Marriage Sex is a powerful force that can destroy if not used properly. Like atomic power, sex is the most powerful creative force given to man. When atomic power is used correctly it can create boundless energy; when it is used i… Read More
  • Diva na Hudda bifu bado? Kama utakua ni muumini wa twitter lazima utakuwa unajua kinachoendelea kati ya mshiriki wa BBA kutoka Kenya  (2013), Huddah na mtangazaji Diva Loveness love. kiufupi ni tweef ( bif kupitia twitter) kisa kikiwa ni CMB… Read More
  • Msaada ............ Nataka kuvunja ndoa kisheria Habari zenu Wadau wa  Extreme79! Natumai mu wazima na mnaendelea vyema kulisukuma gurudumu la maendeleo.  Naomba msaada wetu katika hili.........Mimi ni mume wa mtu niliyefunga ndoa mika 6 iliyopita,… Read More
  • Wiz Khalifa and Amber Rose are married? Just married! Wiz Khalifa and Amber Rose secretly tied the knot in Los Angeles on Monday  Big news: The 25-year-old rapper was the first to announce the happy news on his Twitter page Overjoyed: Only mome… Read More

0 maoni: