Wednesday 13 November 2013

Kuna ukweli wowote katika hili?.... Mbunge wa Gairo anamtumia Rose Mhando kumkusanyia wananchi jimboni

Katika hali la kudhihirisha namna alivyochokwa na jamii, Mbunge wa Gairo Ahmed Shabiby anaendesha operesheni ya kujitakasa kwa wananchi huku mikutano yake ikipambwa na mwimbaji wa nyimbo za Injili Rose Mhando.  Tangu wiki iliyopita Mbunge huyo amekuwa akitembelea kata mbalimbali akiambatana na Mhando ambaye anaonekana kupendwa sana na wananchi na hivyo watu kujaa katika show zake za bure, lakin pale tu anapomaliza kuimba, watu huanza kutawanyika kwa kuwa hawana hamu kabisa na Mbunge huyu mwenye sifa za ubabe, uonevu, majivuno na mnyonyaji.

Mara zote amekuwa akijisifu kwamba yeye ndiye anayetoa pesa kuendesha miradi mbalimbali kama maji, barabara, shule, zahanati na hata ujio wa wilaya mpya ya Gairo yeye ndiye aliyeileta. 

Kwa kawaida Rose Mhando hutoza si chini ya Tsh 3mil kwa show moja. Wananchi wa Gairo wajihoji, Je haya ndo matumizi ya Fedha zao za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo? Je matatizo yao yatatatuliwa kwa staili hii?



Kwa hisani ya Mpanda Jr

0 maoni: