Sunday, 10 November 2013

KASEJA atua YANGA

Mlinda mlango nambari moja nchini Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka 10 mfululizo Juma Kaseja Juma jana majira ya saa 2 usiku alisaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Young Africans yenye makao yake Twiga/Jangwani kwa kipindi cha miaka miwili.Usajili wa Juma Kaseja kujiunga na klabu ya Yanga unafuatia mapendekezo ya benchi la ufundi katika ripoti waliyoikabidhi kwa kamati ya mashindano kwa ajili ya kuboresha kikosi kwa ajili mzunguko wa pili na mashindano ya kimataifa.
Benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Ernie Brandts lilihitaji mlinda mlango mwenye uzoefu wa michezo ya kimataifa kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kimataifa na mzunguko wa pili ambao utakua na upinzani kulingana na kila timu kutaka kufanya vizuri.
Akiongea na www.youngafricans.co.tz mara baada ya kumalizika kwa zoezi hilo mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Yanga Abdallah BinKleb alisema hawana shaka na uwezo wa Kaseja kwani rekodi yake ndani na nje ya nchi inafahamika kwa hiyo wanaamini atatoa mchango mkubwa wa timu ya Yanga.
Timu yetu imekamilika kila idara, kikubwa tunachokifanya ni kuhakikisha tunazidi kukiboresha na kuyafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi ili kuhakikisha Yanga inaendelea kufanya vizuri na kutisha katika Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
"Najua wegine watajiuliza maswali mengi kwa nini Yanga wamemsajili Kaseja, ukweli ni kwamba walinda mlango waliopo ndani ya Tanzania Kaseja bado ana uwezo nkubwa na msaada ambao atautoa katika kukiimarisha kikosi chetu" alisema Bin Kleb
Kaseja hakua na timu yoyote aliyoichezea katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na timu yake ya zamani ya Simba SC hivyo kujiunga na Yanga kama mchezaji huru katika kipindi hichi cha drisha dogo la usajili.
Kutua kwa Kaseja kunaifanya Yanga kuwa na walinda mlango wanne wote wenye uwezo wa hali ya juu na kutokuwa na shaka wakati wowote timu inapokuwa inakabaliana na mashindao yoyote iwe ni ndani ya nchi au ya nje ya nchi (kimataifa).
Kaseja anaungana na walinda mlango wengine Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul ambao wataitumikia klabu ya Yanga kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom januari 2014 na mashindano ya klabu Bingwa Afika 2014. 
Kwa hisani ya www.youngafricans.co.tz

Related Posts:

  • Madawa ya Kulevya yamfilisi AISHA MADINDA WIMBI la uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya limeshika kasi hivi sasa kwa wasanii na watu mbalimbali huku Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe akilivalia njuga kulikomesha.Wakati hayo yakiendelea, mnenguaji aliyetik… Read More
  • Kaseja: sijasaini Lupopo, bado naipenda Simba KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja amesema hajasaini mkataba wa kuichezea FC Lupopo ya DR Congo ila wapo kwenye hatua nzuri ya mazungumzo lakini akasisitiza kuwa bado ana mapenzi na klabu yake ya zamani ya Simba. Ka… Read More
  • Malinzi achukua fomu ya urais TFF ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Yanga SC, Jamal Malinzi amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27, mwaka huu. Fomu hi… Read More
  • Kaseja akumbwa na balaa lingine! Rais Lupopo amuita paspoti yake yaibwa KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja, ameendelea kukumbana na mikasa lukuki baada ya paspoti yake kuibwa katika hali ya utatanishi huku rais wa Klabu ya FC Lupopo, Victor Kasongo Ngoy, akimtaka aende DR Congo wiki hii.&nb… Read More
  • Biggest Beauty No-No's Christina hit the great trifecta of beauty fails with this one: over bronzed, invisible brows and sparse spider lashes. …to over powdering. Blend, blend, blend! Keep your lipstick from bleeding with an outer liner i… Read More

0 maoni: