Tuesday, 29 October 2013

Kweli Mjini shule! Hebu soma kioja cha Mhudumu wa basi la Ngorika na abiria wake ......

Juzi siku ya j’mosi nilikuwa nasafiri kutoka Simanjiro kwenda Mkoa K’njaro. Nilipomaliza shughuli zangu Moshi nikaamua kwenda Mkoa wa Arusha kwa ndugu ambayo ilinilazimu kupanda basi la kuanzia Moshi au yale mabasi ya Mikoani . Kwa sababu mabasi ya mikoani hayasimami mara kwa njiani nikaamua kupanda basi la Ngorika na kupata kiti cha mwisho ktk gari hilo.
Hivyo safari ikaanza kwenda Ars basi ilipofika eneo la mailisita Mhudumu wa Kike akafika eneo tulipo akiwa amevaa miwani mkononi amepakata kitabu cha tiketi au risiti na kalamu Akaanza kuandika tiketi na kukikata na kudai na nauli kwa kusema “HAPO WEWE” nilifikiri sana mambo mengi kichwani kuwa huyu mhudumu angalau amefuzu mafunzo VETA ili kufanya kufanya kazi hii muhimu .

Pili kazi inafikirika kuwa na ubavu wa kufokea wateja au abiria hii ilidhihirika pale nilpomuuliza mbona hii tiketi ulionipa haina namba ya usajili wa gari hili nililopanda ,Alichonijibu namba ya nini? Kwani una shida gani mpaka unaniuliza za gari ,kwanza una begi kwenye buti la gari useme litapotea.

Nami nikamjibu kuwa kila binadamu ana jina lake,na magari yanatambulika kwa namba ya usajili.

Ndipo kwa hasira akachukua tiketi yangu akaandika namba ya gari ambayo ni T768- akanikabidhi tiketi nilpoisoma nikagundua kwamba sio namba sahihi ,Nikamuuliza tena mbona namba hii sio sahihi?

Alichonijibu nyie watu Moshi mnasumbua sana unataka nikubebe mgongoni ,name nikamjibu sikufika huku unaonekana kuwa somo la “customer care hukupata” 

Mwisho akaniambia kama nimekuudhi sana unaweza kwenda ofisi yetu pale Arusha au soma namba gari hapo nyuma baadae hukishuka kwenye basi hili ,Nikamwambia hata mbele kuna namba za usajili wa gari.

Namba la gari lenyewe ni T768 BKW.

Hitimisho langu kwamba Sumatra & TRA wanalijua jambo hili kuwa magari mengi hayatoi tiketi kwa kwa abiria au wakitoa haikuandikwa namba za usajili kwenye tiketi hizo.

Pia wenye magari mnaajiri wafanyakazi wenye taaluma ya usafirishaji au mnaajiri wapiga debe vituo vya mabasi?Madereva wenu huwa na likizo ya kila mwaka?


Kwa hisani ya Mdau MS

0 maoni: