Tuesday, 1 October 2013

Kuna ukweli wowote katika hili?Josephine Mshumbusi unainajisi CHADEMA. Tafadhali na tuchore mstari, tuseme yatosha sasa!


Kama mtu yeyote aliye makini, asiye mbabaishaji mwenye kuheshimu taasisi na utendaji kazi wake lazma atakubali kuwa kwa sasa Chadema ni chama chenye mvuto na wafuasi wengi nchini. Katika kuitaja chadema pia huwezi kutokumtaja Dr Wilbrod Slaa (mzee wetu tunamheshimu sana)Lakini kuna jambo ambalo kwa watu makini htuwezi kupuuzia kisa limefanywa chini ya Mwamvuli wa Dr Slaa. Tunafanya hivi kwa sababu tunaamini Dr Slaa mwenyewe hapendi hivyo sisi km wapenzi wa chadema tunampa justification ya yeye kulikemea.

Mwanamama Josephine Mshumbusi mke wa Dr Slaa (ref presumption of marriage) amekuwa mtu kwa namna fulani niseme amekosa busara sana hasa pale anapojadili maswala ya kichama with authority wakati yeye hana nafasi za kimamlaka CHADEMA na wala katiba ya chadema haijaainisha majukumu ya Mke/mchumba wa mwenyekiti au katibu.

Kwa watu ambao wana hobby ya kuingia sana katika hizi networks (facebook na JamiiForums).. Ukisoma post anazoweka Josephine kama ni mtu MAKINI lazima uta-question hekima yake (kama mwanamke wa kiafrika), lakini hutaishia hapo utajiuliza hivi anaweza kumshauri nini Dr. Slaa?

Kuna wakati watu waliquestion uhaalali wa Dr Slaa kukopeshwa fedha na chama (ofcoz ilikuwa ni propaganda ambayo hata chadema hawakuona umuhimu wa kujibu coz ni jambo lililopitishwa kwenye kamati kuu) lakini alikuja Josephine kuongea maneno sana hapa, mara unajua tunatumia shs ngapi, mara unajua tunasomesha watoto yatima wangapi, mara mshahara anaolipwa Dr hautoshi, etc etc.

Amekuwa akijibu hoja za vijana wa Lumumba ambazo hazina msingi na badala ya kumsaidia Dr. Anajikuta anamvua nguo. Ukienda Tanuru la fikra facebook utakuta anajibizana na Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

Kubwa kuliko jana ZeMarcopolo na Ritz wamemprovoke akaamua kuingia na verified ID ya katibu wa chama Dr W Slaa na moja ya post yake ni hii


"Kwenda na basi AMA ndege siyo tatizo. Tatizo ninaangalia mda na ukubwa wa tatizo. Punguza pumba lini uliniona kwenye bus"

Huyu ni mke wa Katibu wa chama kinachotarajia kuongoza dola. Is this fair? Josephine got to shut up ataonekana na busara kuliko kuja kupost trivial stuffs zinazoreveal kiburi chake na ujinga. Unautia wasiwasi uma wa wana wa hili taifa kuhusu msaada wako kwa Dr. 

Wananchi wa Ileje, makambako, masasi, namnyumbu, katangiri, kibandamaiti, nachingwea wanakuomba kama hoja haikuhusu nyamaza vijana na viongozi wa chadema wajibu. Unawapa kazi nzito vijana wanaokipenda chama kukitetea hapa mtandaoni.



Dr Slaa na wanaCHADEMA najua pengine msingependa kusoma hili bango lakini hatuwezi kunyamaza tunapoona mtu anajaribu kuitia unajisi CHADEMA ambayo wapo watu waliokufa wakiitetea chadema, wengine wamefungwa magerezani, wengine wamepata ulemavu wa kudumu na wengine walikuwa matajiri wakafilisika kisa CHADEMA. 

Chonde chonde Josephine.


Chanzo - 6gates

0 maoni: