Friday, 18 October 2013

Vifo vya Wasanii makubwa yaibuka - Mchungaji adai kuwaua wasanii SHARO, KANUMBA na wengine

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘The Great’. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda.

VIFO MILIONI 605 

Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao.
WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU

Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kundi la Five Stars wapatao 14, Kanumba, Sharo Milionea na mwanamuziki James Dandu ‘Mtoto wa Dandu’. Pia alidai kuwa alihusika katika vita kati ya aliyekuwa Rais wa Iraq, Sadam Hussein na Marekani kwa kutumia pepo la uchonganishi alilolitaja kwa jina la ‘Magweju’. Pia mchungaji huyo alidai kuhusika na  shambulio la hivi karibuni la Al-Shabaab katika maduka ya Westgate la Nairobi nchini Kenya na matukio mengine mengi hadi kufikia idadi hiyo ya vifo vya watu milioni 605.
AWAONEA HURUMA WASANII, AWAONYA

Mchungaji huyo aliendelea kusimulia kuwa alipokuwa katika ulimwengu wa giza aliwahi kuwaonea huruma wasanii kama Kanumba, Sharo Milionea na Mtoto wa Dandu na kuwatokea kimiujiza akiwaonya waokoke kabla ya kuchukua roho zao huku mashabiki wao wakibaki na simanzi wakiamini kuwa vifo vyao ni vya kawaida. Alidai kuwa baada ya kuwafuata mastaa hao na kuwaonya walikataa na badala yake akawaua. Akiendelea kulishuhudia kanisa, Mchungaji Mayanga alisema kuwa kwa sasa ameokoka na kuachana na mambo ya giza, hivyo haogopi kuzungumza ukweli kwa kuwa roho wa Bwana anamuongoza kushuhudia kila kitu alichokifanya ili waumini watambue uwezo wa Mungu.
ANA SIRI NZITO ZA VIGOGO

Huku akiomba hifadhi ya majina ya wahusika, mchungaji huyo alihitimisha ushuhuda wake kwa kudai kuwa ana siri nzito za vigogo au watu wakubwa ambao aliwahi kwa namna moja au nyingine kuwapa utajiri wa nguvu za giza.
UTABIRI

Hata hivyo, baadaye jamaa huyo alijitabiria kuwa atakamatwa na kufungwa siku moja kutokana na siri alizonazo.  “Yaani nina siri za watu wengi sana, nikiwaambia mtaogopa na nchi itatikisika. Najua siku moja watu watanikamata na kunifunga pingu kwa siri nilizonazo, lakini kamwe siogopi kwa kuwa Bwana ananiongoza,” alisema Mchungaji Mayanga.
KANUMBA, SHARO MILIONEA

Kanumba alifariki dunia mwaka jana akiwa nyumbani kwake Sinza-Vatican, Dar huku Sharo Milionea akipoteza uhai kwenye ajali ya gari iliyotokea wilayani Muheza, Tanga wakati msanii huyo akienda kwao mkoani humo akitokea Dar.
Kwa hisani kwa GPL

Related Posts:

  • Redio ya SHAROimenifanya mauzauza MSANII wa Kundi la Green Masage, linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya TBC, Daniel Mmasi ‘Face Brown’ amefunguka kuwa redio ya marehemu Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ aliyoinunua, imemletea mauzauza Akizungumza… Read More
  • Diamond awekeza kwenye ardhi? WAKATI Wema Isaac Sepetu akiongeza idadi ya magari kwa kununua mkoko wa maana, zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemziba mdomo baada ya kununua eneo kubwa ambalo ndani yake kuna nyumba tatu, jirani na anapo… Read More
  • Mmiliki wa Home Shopping Centre hali tete HALI ni tete kuhusiana na tukio la bilionea Said Mohamed Saad kumwagiwa tindikali, athari ni kubwa. Jinsi alivyoharibika inatia simanzi lakini kumpata mhusika wa unyama huo ni kitendawili kinacholitega Jeshi la Polisi Tanz… Read More
  • Meneja wa Wema Sepetu afunguka kuhusu mahusiano yake na Wema MARA  nyingi amekuwa akionekana karibu sana na msanii wa filamu mwenye jina kubwa Bongo, Wema Isaac Sepetu. Ukaribu wao umewafanya baadhi ya watu kuhisi tofauti. Wapo waliosema ni wapenzi kutokana na picha zao za ki… Read More
  • Kaseja: sijasaini Lupopo, bado naipenda Simba KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja amesema hajasaini mkataba wa kuichezea FC Lupopo ya DR Congo ila wapo kwenye hatua nzuri ya mazungumzo lakini akasisitiza kuwa bado ana mapenzi na klabu yake ya zamani ya Simba. Ka… Read More

0 maoni: