Tuesday 29 October 2013

Baby Madaha a.k.a "Queen of Swaggz" azidi kupasua mawimbi......

Nyota ya Baby Madaha a.k.a "Queen of Swaggz"  ilidhihirisha kuanza kung'ara siku ya ijumaa ya 25/10/2013  baada ya kufungua pazia la mafanikio  na kuweka historia  kwa kutambulisha  rasmi moja ya bidhaa zake  "Gift bag" zenye picha zake katika hotel ya Den France iliyopo maeneo ya  Sinza jijini Dar es salaam.

Mwana dada huyo alifanya hafla hiyo fupi iliyohudhuliwa na  watu wa habari, wasanii wa Muziki , ndugu jamaa na marafiki. Kwa kuwaweka watu mkao wa kula inasemekana "Queen of Swaggz  aliyeingia mkataba mnono wa Kampuni ya Cand n' Candy ya Kenya na hivi punde anatarajia kutambulisha  bidhaa nyingine ya   manukato  " perfume" yenye picha zake na kuachia video yake mpya aliyoifanya kwenye mahadhi ya Dance hall inayoitwa MR. DJ

Angalia baadhi ya picha za tukio hapa chini
Baby Madaha afanya party ya kutambulisha Bags zake na Perfume Bongo, Tazama picha jinsi ilivyokuwa.






Stay tune.............

0 maoni: