Wednesday, 23 October 2013

Baby Madaha afanya Mambo KENYA

Mwanadada aliyerudi kwa kasi kwenye gemu la muziki nchini na kuachia ngoma zake mbili kali sana mwaka huu “Squeeze it” na “Summer Holiday”, Baby madaha, ameendelea kudhihirisha kuwa mwaka huu kajipanga Zaidi kusaka hela baada ya hivi karibuni kuachia Perfume na Mifuko yenye jina lake (Brand) huko nchini Kenya.
Akizungumza kwa simu tokea nchini humo ambako yupo akijiindaa kufanya tour yake ya kwanza baada ya kupata Mkataba na Kampuni ya Candy n Candy records ya nchini humo, Baby Madaha amsema perfume hizo zimeshaanza kuuzwa na kupatikana katika mitaa na maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na amesema kuwa mzigo wa pili utatua Tanzania hivi karibuni.
“Nimeona  bora nianze na Kenya kwanza kwasababu nimegundua kuwa huku nina mashabiki wengi sana Zaidi hata ya bongo, hata siamini kinachotokea” Alisema baby Madaha.

Angalia picha ya baadhi ya bidhaa zake hapa chini
Baby Madaha afanya mazito Kenya, jionee hapa! Hatari Sana!
Kwa hisani ya Bongomovies

0 maoni: