Monday, 28 October 2013

Baba wa DIAMOND adhihirisha mapenzi yake kwa WEMA ......asema “Wema ni mwanamke mwenye nyota kali sana na anapendwa na wengi. Siyo kama hao akina sijui Penny

Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa amejikuta akiangua kicheko ‘hevi’ baada ya kusikia taarifa za mwanaye kurudiana na aliyekuwa zilipendwa wake, Wema Isaac Sepetu. Akizungumza na mwanahabari wetu juzikati, Baba Diamond alisema alifurahishwa mno na hatua ya mwanaye kurudiana na Wema kwani ndiye mwanamke anayejielewa na ana nyota kali tofauti na warembo wengine aliowahi kuwa nao.

“Wema ni mwanamke mwenye nyota kali sana na anapendwa na wengi. Siyo kama hao akina sijui Penny (Penniel Mungilwa).
“Hana majivuno hata mimi nilisema mwanzoni walipoachana kuwa Diamond alipoteza bahati lakini sasa naamini atafika mbali zaidi kwani kama siyo kuachana kwao, Diamond angekuwa mbali,” alisema.
Hata hivyo, alimtaka Diamond kutulia na Wema kwani ndiye mwanamke sahihi kwake na aepuke kutangatanga kwani atashindwa kufanya mambo ya maana yatakayomuwezesha kuwa juu zaidi ya hapo alipo kwa sasa.
Hivi karibuni Diamond alithibitisha kurudiana na Wema wakiwa China lakini alipotua Bongo akaendelea na uhusiano wake na Penny hivyo kuwaacha mashabiki wake njiapanda.

Kwa hisani ya GPL

0 maoni: