Wednesday, 18 September 2013

Sakata la kufungwa kwa Unga AISHA BUI aibuka na kuweka wazi

HUKU kukiwa na madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui amekamatwa na kufungwa nchini Brazil kwa kunaswa na unga, mwanadada huyo ameibuka na kufafanua juu ya tuhuma hizo. Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu kutokea Brazil, Aisha alisema ameshangazwa na madai hayo wakati yeye yuko nchini humo akiwa amemfuata mchumba wake ambaye jina lake hakuwa tayari kulianika.


“Jamani hayo madai ya kwamba nimefungwa huku kwa kesi ya madawa ya kulevya mimi mwenyewe nayashangaa. Niko huku kwa mwezi wa nne sasa, nimekuja kwa mchumba wangu. Hizo taarifa za kwamba eti nimefungwa ni uzushi unaotengenezwa kwa nia ya kunichafua tu.



“Wakati naondoka Tanzania ilikuwa kimyakimya kwa kuwa nilijua kuna baadhi ya watu watazusha mambo ya kunipaka matope na ndicho walichokifanya. “Naomba Watanzania wajue niko huru kabisa, naendelea na shughuli zangu kama kawaida. Natarajia kurudi Bongo hivi karibuni,” alisema Aisha.


Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • Diamond avunja rasmi ndoa ya Irene Uwoya JAMBO limezua jambo, lile sakata la kunaswa hotelini kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Irene Uwoya limezaa matunda hasi kwa ndoa ya mwadada huyo ambayo sasa imevunjika rasmi, Amani limetonywa. Habari ya wawili hao kunas… Read More
  • Sinta na Mange wana bifu? Soma hapa chini Sinta Mange MANENO YAMKOSAJI NI SAWA NA MFA MAJI EEEEH I THINK WENGI WETU TULIAMUA KUMU IGNORE TU HUYU MBWA KOKO......KAMA MIMI NDO KABISAAAAA YANI NILIKUWA NISHASEMA NGOJA NIFANYE KAMA HAYUPO HAI...... JAMANI KIL… Read More
  • Umaarufu kazi ........... Mmmmm haya mambo mengine  kiukweli hata hayakuaga utamaduni wetu ila sasa hivi imekuwa kama lazima... tuongee ukweli haya mambo ya kufanya sherehe za kuzaliwa eti birthday party  yalikuwepo? au ndio kuiga t… Read More
  • Jack Chuz aolewa...... Kila la heri..................... … Read More
  • Baada ya Maisha kumgonga Mwinyi ampigia Magoti Jay dee Ama kweli ujanja mwingi mbele giza.......... na ile methali inayosema  usitukane wakunga na uzazi ungalipo imeanza kufanya kazi katika maisha ya Mwanamuziki wa zamani wa Machozi Band , aliyefahamika kwa jina la  … Read More

0 maoni: