Rehema Chalamila ‘Ray C’ akiwa na Lord Eyez enzi hizo.
INAWEZEKANA umekuwa ukisikia vitu vingi kuhusu lejendari wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ lakini hukupata chansi ya kumsikia mwenyewe akifunguka mwanzo mwisho juu ya kisanga kilichompata alipojikuta kwenye janga la matumizi ya dawa za kulevya.
Ijumaa Wikienda limefanya naye mahojiano (exclusive interview) ambapo amekidhi kiu yako ya kujua chochote kinachomhusu. UNGANA NAYE…
KWA MTU ASIYEKUJUA, UMETOKEA WAPI?
“Nimezaliwa Mei 15, 1982 mkoani Iringa. Kabla ya kuingia kwenye muziki nilifanya kazi ya utangazaji. Watu wengi walinijua wakati nikiwa Radio Clouds FM. Albamu yangu ya kwanza ni Mapenzi Yangu niliyoitoa mwaka 2003. Kilichofuata ni kujipatia mashabiki wengi sana ndani na nje ya nchi. Baadaye niliachia Albamu ya pili ya Na Wewe Milele ya mwaka 2004. Nilipata mialiko mingi nje ya nchi zote Afrika Mashariki, China, Uingereza na kwingineko. Kilichofuata ni singo kibao na tuzo hadi nilipopata matatizo mwaka jana. Unazikumbuka Mama Ntilie, Mahaba ya Dhati, Touch Me, Na Wewe Milele, Wanifuatia Nini na Nihurumie? Huyo ndiye Ray C mwenyewe.
MARA YA MWISHO KUONEKANA STEJINI NI LINI?
“Mara ya mwisho kufanya shoo au kuonekana stejini ni Julai, mwaka jana. (anawaza kidogo) Nakumbuka ilikuwa Nairobi Carnival nchini Kenya. Ilikuwa shoo ya kampuni moja ya simu. Nilifanya vizuri sana aisee. It was wonderful.
UTARUDI LINI STEJINI?
(Akiwa Studio za THT na Prodyuza Tudd Thomas na Imma The Boy anarekodi wimbo) Nipo chini ya management (usimamizi) wangu wa mwanzo kabisa wa Ruge Mutahaba. Ruge ni mtu ambaye anajua kumsimamia mtu. Siwezi kumwangusha amefanya kazi kubwa ya kunisimamia. Ni kama baba kwangu. Nina singo mpya kama 4 au 5. Naandaa albamu itayokuwa na ngoma zote kali nilizofanya kwa takriban miaka 10 sasa itaitwa The Best of Ray C. Itakuwa na greatest hits zangu zote nilizofanya kwa kipindi chote hicho. Tumuombe Mungu. Akinijali na kama mipango itaenda vizuri, Desemba mwaka huu nitarudi rasmi stejini. Nitafanya shoo maalum kwa mashabiki wangu. Nitakuwa na nyimbo mpya kali na zile za zamani. Sipati picha kwa watu watakaohudhuria kwani watapata burudani adimu kutoka kwangu.
UMENENEPA SANA NA ULISIFIKA KWA MAUNO STEJINI HADI UKAPEWA JINA LA KIUNO BILA MFUPA. JE, BADO YAPO?
(huku akijinafasi studio) “Hapa hapatoshi ningetoa shoo ya kufa ya mtu. Mauno yapo ya kutosha. Kiuno lainiii…)
SAUTI VIPI?
“(anapandisha sauti nyororo na kuimba moja ya ngoma zake kali zijazo) Umesikia kitu hicho? Sauti bado ipo vizuri mno.”
WATOTO WADOGO WANAKUJA KWA KASI KWENYE GEMU, INAKUPA PICHA GANI?
“Chalenji ni kubwa lakini lejendi atabaki kuwa lejendi. Tumelitoa hili gemu mbali. Nafurahi kuona wadogo zetu wanafuata nyayo zetu na wanafanikiwa. Nafarijika nikimuona Recho wa THT (Winfrida Josephat) anafanikiwa kupitia aina ya muziki niliyoianzisha mimi. Hainipi shida zaidi ya kufurahia kuwa nimemkomboa mwanamke mwenzangu naye anapata shavu na kuweza kuendesha maisha.”
WEWE NI KATI YA WASANII WALIOPATA USIMAMIZI MZURI TANGU MWANZO, NINI KIMETOKEA?
“Ni kweli mwanzoni nilikuwa chini ya menejimenti ya Smooth Vibes. Ilipofungwa au ilipobadilika, niliamua kujitegemea. Nimekaa kwa zaidi ya miaka 6 au 7 bila kusimamiwa na mtu. Kama ulisikia nipo chini ya usimamizi fulani haikuwa rasmi. Sasa nimerudi kwa Ruge. Naamini nitafanya mapinduzi tena katika muziki huu ili ufike mbali zaidi.”
UMEFANYA KOLABO NA MSANII YEYOTE KWA HAWA WALIOIBUKA MIAKA YA HIVI KARIBUNI?
“Nawakubali sana na tayari nimefanya mazungumzo nao. Nashukuru wakikutana na mimi wananiita lejendi. Wananipenda (anaingia Ben Pol, Ray anatabasamu). Nimepanga kufanya kolabo na Ben Pol (kicheko, wanakumbatiana). Pia nitafanya na Diamond (Nasibu Abdul), anafanya vizuri sana, namkubali. Nitafanya na Recho THT na Ommy Dimpoz (Faraji Nyambo) pia.”
WIMBO WAKO WA MWISHO KABLA YA MATATIZO NI UPI?
“Ni Moto Moto niliofanya na akina Red San na Nonini wa Kenya. Sikuupeleka redioni nchini Tanzani lakini ukiingia mtandaoni kwenye You Tube utaona imesikilizwa na kutazamwa na mashabiki zaidi ya 348,142 hadi sasa.
Kwa hisani ya GPL ...........Itaendelea wiki ijayo.
0 maoni:
Post a Comment