Ninaandika, ninaandika kwa hoja na vigezo, lakini pia kwa nukuu na viambatanisho.
Nitaanza na Nukuu ya Mmoja wa Mitume ya MUNGU ambae aliwahi kusema kuwa "..UKIONA JAMBO LIMEEGEMEZWA (KUPEWA) KWA MTU AMBAE HANA UJUZI NALO BASI TEGEMEENI MAAFA.."
Ninaandika kuwa hali ilipofikia kwa sasa ni wazi kuwa Bunge letu tukufu la jamhuri ya muungano wa Tanzania limenajisiwa. Na katika hili ni lazima kila mmoja atafakari kwa kina na kisha kuchukua uamuzi. Chanzo cha vurugu hizo zilishatajwa hapo nyuma na baadhi ya wenye kusema, kuwa moja ni;- umbumbumbu wa wabunge wapya wa upinzani ambao hawafahamu kanuni na taratibu zinazosimamia na kuratibu bunge, lakini ya pili ni external kuwa kuna nguvu kubwa na msukumo wenye ushawishi wa Pesa kutoka mataifa ya nje ambao wabunge wetu wa upinzani wanapewa ili kuvuruga Amani yetu na kuiingiza nchi kwenye vurugu na kuishushia heshima yake lakini zaidi kuleta dalili za machafuko yasiyo na sababu.
Lakini lipo kosa kubwa ambalo wananchi nao wamelifanya, na nasema hivyo kwa kuheshimu na kuitambua nafasi ya wananchi kama chimbuko la mamlaka zote ikiwemo bunge na wabunge wake. Wananchi ndio wenye dhamana ya kuchagua ni nani awe mwakilishi wao bungeni. Na hapa ndipo nataka tukubaliane kuwa tumechagua vibaya, kwa maana hatukuzingatia na hatukuwa makini kuangalia ni mtu wa aina gani tunamchagua, na kwamba anakidhi vigezo..?
Bila kujipa usumbufu wa kuwachunguza kwa undani wabunge wengi wa upinzani, wakiongozwa na Sugu na Mbowe ni watu ambao hawafai kupewa dhamana ya uongozi na hasa uwakilishi wa watu kama Ubunge ama Udiwani, hawafai, hawana vigezo, kuanzia kwenye malezi yao kifamilia, kielimu na kimaisha kwa ujumla.
Sugu anafahamika kuwa ni miongoni mwa vijana waliokulia kwenye vikundi vya wahuni na akifanya muziki wa kuhamasisha vurugu na matumizi ya mihadarati, baadhi ya mashairi katika nyimbo zake kama mikononi mwa polisi na sugu moto chini ni viashiria vya haya ninayoyaongea hapa. Kwa experience aliyonayo kama kiongozi wa vikundi vya wahuni wa mtaani na watumiaji wa mihadarati hatupaswi kushangaa kwa haya ambayo tunayaona yakitokea bungeni, hayatokei kwa bahati mbaya ni mambo ambayo ndio wanayoyajua na wanayoyaishi, vurugu na ubabe.
Kwa Kiongozi wa kambi ya Upinzani nae ni majanga ya mwaka, kwani elimu yake ambayo ameihitimu vizuri ni ya uchanganyaji wa ala za muziki na nyimbo, ameyaishi maisha haya miaka yake yote, hakuwai hata kuwa kiranja wa darasa katika umri wake wote, hivyo inapotokeA AMEPEWA UONGOZI AMBAO HANA UJUZI NAO Ndio tunaona haya ambayo tunayaona yanaendelea bungeni,. alijaribu kutokimbia umande ambapo alifanikiwa kufika kidato cha sita kwa mbinde lakini kwa bahati mbaya akaambulia kupata division zero. Si kosa lake ni makosa ya waliompa dhamana hiyo, kwa maana hana uwezo nayo na haimudu, yaani ni zaidi ya punga kubebeshwa ngamia, dhamana kubwa sana kwa mwenye maarifa kidogo sana lazima haya yatokee.
Nitoe wito kwa wananchi wenzangu kuwa, tumeshakosea na hilo halina ubishi lakini waswahili wanasema mfanya kosa si kosa bali mrudia kosa ndie mkosaji HIVYO TUSIRUDIE KOSA NA TUKAJUKA KWA KUWA WAKOSAJI.
Kwa hisani ya - TandaleOne
0 maoni:
Post a Comment