Sunday, 29 September 2013

Jasiri haachi asili - Mfungwa anaswa akijiuza !

BAADA Mei mwaka huu kuhukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la kufanya ukahaba, mkazi wa jijini Dar, Blandina Barton amekamatwa tena kwa kosa  hilohilo ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kumaliza kifungo chake, Risasi Jumamosi linakupa mkasa mzima. Habari za uhakika zilizopatikana katika Mahakama ya Jiji, Dar es Salaam zinasema kwamba mfungwa huyo alitumikia kifungo chake katika Gereza la Segerea jijini Dar na alipobakiza miezi michache kumaliza alionewa huruma na bibi jela na kutakiwa kumalizia kifungo hicho uraiani.


Inadaiwa kuwa kabla ya kuachiwa, bibi jela alimsihi Blandina kuhakikisha harudii kosa lililompeleka gerezani pindi atakapokuwa akimalizia kifungo chake nje ya gereza.

Blandina akamhakikishia bibi huyo kwamba atakuwa mtu safi kwani amejifunza vya kutosha.Katika hali ya kushangaza, Jumatano iliyopita Blandina alipandishwa tena katika Mahakama ya Jiji iliyopo Barabara ya Sokoine jijini Dar akiwa amerudia kosa lililompeleka Segerea miezi michache iliyopita.

Imeelezwa mahakamani hapo kwamba, Septemba 24, mwaka huu Blandina na wenzake wanne walinaswa Buguruni usiku wakiwa katika mawindo ya ukahaba. Bahati mbaya kwa Blandina alipofikishwa mahakamani hapo alikutana na hakimu yuleyule aliyemhukumu kifungo cha miezi sita kwa kosa la ukahaba.

Hakimu huyo, Timothy Lyon alipigwa na butwaa baada ya kumuona Blandina akiwa amesimama mbele yake. Mtuhumiwa huyo aliyekuwa na wenzake, Husna Amos, Monica Denis, Esther Chizai na Angela Emmanuel wote kwa pamoja walisomewa mashtaka yao na kukana.

Hakimu Lyon aliwaambia watuhumiwa hao kwamba dhamana iko wazi na kuwataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili na shilingi laki mbili. Sharti hilo lilionekana kuwa gumu kwa watuhumiwa wote, hivyo walipandishwa karandinga na kupelekwa Gereza la Segerea mpaka Oktoba 15, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Mei mwaka huu gazeti dada na hili la Ijumaa liliandika habari za kifungo cha Blandina mara baada ya kuhukumiwa kwenda jela huku ikidaiwa kwamba msichana huyo ni mchumba wa mtu.


Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • WASTARA apata mguu mpya wa bandia STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma Jumamosi iliyopita alikwea pipa kuelekea nchini Kenya ambako ana ziara ya siku nne kikazi na akiwa humo alipata fursa ya kupewa mguu wa bandia bure na wenyeji wake huku pia akiahidi… Read More
  • Madeni ya Harusi yamtesa CHAZ BABA! SIKU chache baada ya kufunga ndoa, Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Baba ‘Chaz Baba’ ameingia kwenye mateso ya kusumbuliwa na madeni yaliyotokana na harusi hiyo. Akizungumza na mapaparazi wa Amani kat… Read More
  • Je tutafika? Watoto wadogo waoana! HAKUNA lugha inayofaa kutumika katika habari hii zaidi ya kusema hii ni kali ya mwaka! Katika hali ya kushangaza, watoto Mary Chinjendi (15) na Amos Sailowa (17), wazaliwa wa Kijiji cha Vilundilo Mbandee, Mkoa wa Dodoma, w… Read More
  • CHID BENZ ndani ya bifu n KASSIM WASANII wanaotamba katika muziki wa Bongo Fleva, Kassim Mganga na Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ juzikati ilikuwa nusura wazichape baada ya kumwagiana matusi hadharani. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni nje ya Ukumbi wa … Read More
  • Watiwa Mbaroni dakika 3 baada ya kufnga ndoa JESHI la polisi nchini limefanikiwa kuisambaratisha ndoa ya mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mboga iliyopo Chalinze mkoani Pwani, Asha Daru mwenye umri wa miaka 15, aliyeozeshwa kwa Said Ally (29),… Read More

0 maoni: